Wakuu ningependa tujadili kauli ya katibu wa nishati na madini aliyoitoa jana kupitia ITV habari wakati akielezea sababu ya kutembea na baadhi ya vitu alivyoibiwa ikiwepo passport na vitu vingine, kuna kauli aliyoongea ambayo ni "VIPESA" kwamba analazimika jutembea na vipesa kidogo ambazo zilikuwa TZS 1,000,000 pamoja na dollar 4,000. Je kauli ya vipesa ni kiswahili ambacho kipo au ni kauli ya zarau?
Karibuni mtoe hoja
Kweli Baba Riz anawasaidizi makini sana
kuna mijitu mingine mnadharau za kishambaKwa asiyejuwa Kiswahili kusema vijipesa au vijisenti inakuwa ni mwao, kwa Waswahili ni neno la kawaida kabisa na hata ukitembea na mabillioni inatakiwa usijikwaze kwa kusema natembea na "mapesa" au "mabillioni". Hata bwana "mapesa" aliomba msamaha wakati fulani kwa kauli yake hiyo. Nna uhakika wote ambao mnashangazwa na hilo neno, Kiswahili si lugha mama kwenu. "Nimejidundulizia vijisenti vyangu nikajijengea kibanda changu mtaa wa Mahiwa", Kumbuka hiyo ni prime area Kariakoo Dar. Na hilo ni jumba la vyumba sita ambalo kiwanja tu kwa sasa ni millioni 800. Ni utamu wa Kiswahili.
kuna mijitu mingine mnadharau za kishamba