Katibu wa Chadema wilayani Serengeti aicha CHADEMA kwenye mataa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Julius Anthony, katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, amejiuzulu baada ya kutuhumiwa kusababisha mgombea udiwani wa chama hicho kata ya Ikoma, Kenedy Josephat kutopitishwa kuwania udiwani.




Wakati Anthony akichukua uamuzi huo, uongozi wa wilaya na mkoa wa chama hicho unatarajiwa kuketi leo Jumatatu Julai 16, 2018 kujadili sababu za Josephat kushindwa kuwasilisha fomu za uteuzi.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Porini; diwani wa Kata ya Nyansurura, Francis Garatwa na baadhi ya wanachama wa Chadema wanamtuhumu Anthony kuwa aliandika barua za Josephat kimakosa na kusababisha ashindwe kupitishwa kuwania udiwani.



Wamesema aliandika barua ambayo haina tarehe, fomu kutokuwa na muhuri wala sanni huku bahasha iliyokuwa na barua hiyo ikiandikwa kwenda kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Ikoma, huku barua ikieleza kuwa inakwenda kwa msimamizi wa jimbo.



Wamesema licha ya Anthony kurekebisha mara tatu bado tarehe ya uteuzi aliandika Julai 14 wakati ulikuwa Julai 12, kudai makosa hayo yalikuwa ya makusudi ili kumwezesha mgombea wa CCM, Michael Kunani kupita bila kupingwa. Kunani alikuwa diwani kata ya Ikoma kwa tiketi ya Chadema, mwanzoni mwa mwaka huu alijiunga na CCM.
Katika barua yake ya Julai 15, 2018, Anthony amesema amejiuzulu uongozi kwa hiari yake kutokana na tuhuma anazopewa.



“Nimechukua uamuzi huu kutokana na Porini kutengeneza mvutano na mgawanyiko miongoni mwa madiwani wa Chadema ambao umesababisha madiwani wawili wa kata ya Ikoma na Manchira kujiunga CCM,” amesema.



Akijibu hoja hizo, Porini amesema sababu zilizotolewa hazina mashiko: “Ameamua kukimbia kabla ya hatua kali hazichukuliwa dhidi yake maana ameachia ngazi baada ya kubainika kukihujumu chama.”
 
Back
Top Bottom