Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Mimi mtazamo wangu tuanze kuchukua mzuri ktk rasimu ya warioba tuweke kwenye katiba iliyopo na tutondoe vipengele vya hovyo ktkt katiba yaliyopoMchakato wa katiba mpya ulikwama. Bado Tanzania ina uhitaji wa Katiba mpya. Kama nchi, ili kupata Katiba mpya mwaka huu au hata ujao, tuanzie wapi ili kusonga mbele?
Karibuni kwa mjadala
- Tuanzie kwenye Katiba Inayopendekezwa na kuendesha Kura ya Maoni? Hapa tutahitaji mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazosimamia Kura ya Maoni kwakuwa kisheria, mchakato ulishakwama, yaani, muda wa kufanyika mambo mengi ulishapita.
- Tuanzie kwenye Raismu ya kwanza au ya pili ya Tume ya Jaji Warioba? Hapa patahitajika kuundwa tena kwa Bunge Maalum la Katiba na mjadala kufanyika tena. Mjadala na mchakato utakapokamilika, Katiba Inayopendekezwa itapatikana na kupigiwa kura.
- Tuanzie kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba? Yaani, mchakato wa Katiba mpya uanze upya kabisa?
Tuanzie pale BOSS na MFADHILI Wa Chadema, LOWASSA,KINGUNGE,MAHANGA na Crew nzima ya FISADI LOWASSA Ilipopiga KURA YA NDIYOOOOOOOOOOO KWA IBARA ZOTE ZA KATIBA PENDEKEZWA,Na kutuletea katiba pendekezwa.Mchakato wa katiba mpya ulikwama. Bado Tanzania ina uhitaji wa Katiba mpya. Kama nchi, ili kupata Katiba mpya mwaka huu au hata ujao, tuanzie wapi ili kusonga mbele?
Karibuni kwa mjadala
- Tuanzie kwenye Katiba Inayopendekezwa na kuendesha Kura ya Maoni? Hapa tutahitaji mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazosimamia Kura ya Maoni kwakuwa kisheria, mchakato ulishakwama, yaani, muda wa kufanyika mambo mengi ulishapita.
- Tuanzie kwenye Raismu ya kwanza au ya pili ya Tume ya Jaji Warioba? Hapa patahitajika kuundwa tena kwa Bunge Maalum la Katiba na mjadala kufanyika tena. Mjadala na mchakato utakapokamilika, Katiba Inayopendekezwa itapatikana na kupigiwa kura.
- Tuanzie kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba? Yaani, mchakato wa Katiba mpya uanze upya kabisa?
Duh!! Hapa nikama una agenda tofauti na mjadala uliotakiwa. Nadhani bunge linaweza kukaa siku za karibuni, wanajua ni nini kinatakiwa sasa. Ningekuwa mimi nimepata fursa ya kushauri ningeshauri liundwe bunge maalumu la katiba ili iletwe rasimu iliyoridhiwa na pande zote!!Tuanzie pale BOSS na MFADHILI Wa Chadema, LOWASSA,KINGUNGE,MAHANGA na Crew nzima ya FISADI LOWASSA Ilipopiga KURA YA NDIYOOOOOOOOOOO KWA IBARA ZOTE ZA KATIBA PENDEKEZWA,Na kutuletea katiba pendekezwa.
Mchakato wa katiba unaendeshwa kisheria sio kimjadala jamii forums.Kisheria bunge la katiba lilishaitishwa na kuipitisha rasimu ya katiba na lilishavunjwa.Watu tunasubiria kuitishwa kura ya maoni tuikubali au tuikatae hiyo rasimu iliyopitishwa na bunge la katiba.Hizo zingine porojo.Watu waliambiwa wabaki bungeni wajadili wakatimuka.Process hairudi nyuma tena sheria hairuhusu itakuwa uvunjifu wa sheria.
Haujasimama ulisimama kusubiri uchaguzi upite na Serikali iundwe.Imeshaundwa ya muungano kinachosubiriwa ni Zanzibar wamalize mambo yao ya uchaguzi sababu kuna maswala yatatakiwa yashughulikiwe na serikali ya Zanzibar na baraza la wawakilishi itakayochaguliwa.Pande zote serikali zikishakuwepo ndipo mchakato huu utaendelea kwa kuitisha kura ya maoni.Kwa machakato ulipo, hata mbele hauendi. Hapo unasemaje?