Katazo la matumizi mifuko ya plastiki

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
Hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko aina ya plastiki maarufu kama ‘rambo’ inayotumika kubebea bidhaa.
Katazo hilo lililotangazwa bungeni jijini Dodoma Aprili 9, 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa tayari limeanza kutekelezwa na ifikapo Juni mosi, 2019 ni mwisho wa matumizi yote ya mifuko hiyo.

Katika kusimamia katazo hilo na kuhakikisha linatekelezwa kwa ufanisi, Ofisi ya Makamu wa Rais yenye dhamana ya kusimamia utunzaji wa Mazingira imeunda kikosi kazi ambacho kinaundwa na taasisi mbalimbali za Serikali.
Ni heri kuzuia kuliko kuponya hivyo Serikali imechukua hatua za kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo ili kuepusha athari mbalimbali za kiafya zinazoendelea kujitokeza.
Imezoeleka kutumika kwa mifuko ya plastiki kubebea bidhaa mbalimbali hususan za vyakula bila kujali athari za mifuko hiyo kwa afya za binadamu, wanyama na mazingira.
Mifuko hii baada ya matumizi imekuwa ikitupwa ovyo na hata ikitupwa kwenye mashimo ya taka huweza kupeperushwa kwa upepo na kusambaa hivyo husababisha uchafuzi wa mazingira. Hata ikichomwa moshi wake una athari kwa binadamu.
Pia mifuko ya plastiki haiwezi kuoza kwa haraka katika mazingira wanadamu walipo kwani inakadiriwa kuweza kudumu hadi zaidi ya miaka 500 na hivyo kuleta athari za muda mrefu n ahata ikichomwa huleta madhara ya kiafya.
Madhara mengine yanayoweza kutokea ni kusababisha mafuriko katika maeneo ambayo kuna mifereji kutokana na kuziba kwa miundombinu ya majitaka na mifereji ya mvua.
Aidha, wanyama ikiwemo mifugo hufa pindi wanapokula na kumeza mifuko hiyo la na kuimeza mifuko hiiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba anafafanua kuwa Serikali inahakikisha katazo hilo linakuwa na nguvu kisheria.
Anasema Serikali imeandaa kanuni za katazo hilo zitakazotangazwa katika gazeti la Serikali chini ya Sheria ya Mazingira na kutoa adhabu ya faini au kifungo kwa mtu atakayekiuka utaratibu uliowekwa.
Waziri Makamba anabainisha kuwa katazo hilo la mifuko ya plastiki si la kushtukiza kwani limekuwa ni shirikishi kwa wada yaani wananchi.
Anasema kuwa Ofisi yake tayari ilisharatibu mikutano katika maeneo kadhaa nchini na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu katazo hilo la mifuko ya plastiki.
Waziri Makamba anasisitiza Serikali itasimamia kikamilifu katazo hilo ifikapo tarehe hiyo ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika kipindi kilichotolewa ni kifupi.
Itakumbukwa kuwa awali Serikali ilitangaza kuzuia matumizi yote ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari mosi, 2017.
Baada ya mashauriano na Shirikikisho la la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na umma ilikubali kusogeza mbele hadi Desemba 31, 2017 ili kutoa muda kwa wajasiriamali, umma na CTI kujiandaa na utekelezaji wa katazo hilo.
Kwa kutambua umuhimu na ukubwa wa jambo hilo, Serikali haikuanza kulitekeleza Januari mosi, 2018 ili kutoa muda wa ziada kwa wadau hao kujipanga zaidi.
Hivyo kutokana na hilo katazo lilisogezwa mbele hadi kufikia Juni mosi, 2019 kama ambavyo imetangazwa na kutoa muda wa kutosha wa matayarisho
Serikali imeunda kikosi kazi kitakachoratibu utekelezaji wa zoezi hilo ambacho kinajumuisha watendaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mapato Tanzaniana Idara ya Uhamiaji.
Taasisi zingine ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Hata hivyo hivyo, Waziri Makamba anawaondoa hofu wananchi kwa kusema kuwa katazo hilo la mifuko ya plastiki halitahusu baadhi ya vifungashio vya bidhaa zikiwemo maziwa, mikate.
Vifungashio vingine ni vya pembejeo za kilimo, ujenzi, dawa na baadhi ya vyakula kama korosho na vinywaji vikiwemo maziwa ambavyo ni ni lazima vikidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


Ng’ombe wakila mifuko ya plastiki iliyozagaa kitengo ambacho husababisha vifo kwa mifugo hiyo na pia haiwezi kuharibika kwa haraka hivyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Mifuko ya plastiki iliyokatazwa matumizi yake.
 
mnakataza wakati mifuko.mbadala hamjaleta! kwa nin msiwaambie wenye viwanda vya mifuko wabadili mfumo bas! eti ukikamatwa na mfuko faini nyie kweli wajinga na waziri makamba yupo kama sio Mtanzania vile khaaa ananata sana mpaka anakera
 
Ni hatua nzuri sana.
Athari za hiyo mifuko ni kubwa kuliko hata matumizi yake.
Pia ni fursa kwa wajasiriamali
 
Tupo pamoja
Vijana changamkieni fursa ya kuleta mbadala wa hii mifuko iliyopigwa marufuku sasa
 
Katazo hili ni jema sana. Japo nimekuwa critical na mambo mengi ya serikali ila kwa hili naunga mkono. Najua kuna watu wanategemea uuzaji wa mifuko hii kuishi nami nawasihi watumie fursa hii kubuni mifuko rafiki kwa mazingira kabla wafanyabiashara wakubwa hawajaanza kuagiza kutoka nje na ushindani ukawazidi nguvu.

Tuna mali ghafi kama katani, matawi ya michikichi, minazi, n.k. ambayo nimepita baadhi ya nchi nikaona watu wakitengeneza vibebea bidhaa kutokana na matawi yake.

Natambua changamoto zilizopo na kushindwa mara nyingi kwa serikali yetu kusimamia matamko yake hasa katika mambo ya msingi nje ya siasa. Ila nawapa benefit of doubt kwa sasa. Mimi nimeacha kuitumia ili nisiwe chanzo cha kushindwa kwa azimio hili. Wewe je?

TUILINDE NCHI YETU, TULINDE WAJUKUU NA VITUKUU WETU.
 
Hili nalo ni matokeo ya kukurupuka kwetu.Mtu anatoa katazo wakati kitu mbadala hakuna.kama hiyo mifuko imetumika miaka yote kilichoshindikana kuanza kutengenezwa kwanza hiyo mbadala ikishasambaa nchi nzima ndo hizo rambo zipigwe marafuku.Hiyo June si kesho kutwa tu au mnataka kuonea watu na matamko yasiyo angalia uhalisia.
 
Tunakimbilia wapi kuleta matamko na makatazo wakati tulikua na uwezo wakufanya hili jambo likakaa vizuri.Watu wangekua na mifuko mbadala wala haya matamko yasingekuwepo kwasababu rambo zingeondoka zenyewe sokoni ila kinachofanyika sasa hivi ni papara na ata kama zoezi litafanikiwa litafanikiwa kwakutumia nguvu nyingi na kuonea watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…