Hapana Mkuu, hii ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi zake zote bila kupiga matuta.
Michuano hii iliyoanza Juni 5, ilishirikisha timu nane, nyingine Nakuru All Stars, Tusker FC za Kenya pia, Jang’ombe Boys ya Kenya, Yanga, Simba za Dar es Salaam na Singida United ya Singida.
Yanga ni timu pekee ya Tanzania iliyofika Nusu Fainali na kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na AFC Leopards baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Jang’ombe Boys ililambwa 2-0 na Gor Mahia katika mchezo wa kwanza, wakati Singida ilitolewa kwa penalti 5-4 na Leopards na Simba ilitupwa nje kwa penalti 5-4 na Nakuru All Stars.
Michuano hiyo mwakani itafanyika Kenya.