pole sana mkuu.
Uwezo hupo mkuu wa kuokoa meno yako ufanye maamuzi haraka sana.
Nenda kwa daktari wa meno wa safishe meno.unatoka damu kwa vile fizi zako azipumui na zimevimba.unatakiwa kwenda kwa daktari wa meno kusafisha japo mara moja kwa mwaka.
Baada hapo wewe binafsi inabidi upige mswaki mara mbili kwa siku kila baada ya mlo tumia mswaki laini.tumia mswaki wako laini kukanda fizi zako taratibu kila ukipiga mswaki.kitu kingine muhimi ni kutoa vyakula vilivyo nasa kati kati ya meno (flossing).kwa vile fizi zimevimba kwa sasa inabidi baada ya yote hayo huwe unasukutua na maji ya chumvi ya vugu vugu kila baada kupiga mswaki.piga mswaki kabla kwenda kulala na usile kitu kingine unaweza kunywa maji.
Ukifatisha yote hayo mkuu na atakayoongezea daktari wa meno hutopoteza meno yako na wala kuona tone la damu wakati wa kupiga mswaki.
ni usafi wako tu unahitajika hapo.si lazima umwone dakta wa meno,sukutua meno yako sawia kabla na baada ya kula,sugua fizi na ulimi,osha kwa maji ya chumvi mara kadhaa,chokonoa fizi zako kutoa mabaki ya chakula na nyama nyama ktk fizi ............,Jamani wana jf doctor nisaidieni nisijekuwa kibogoyo.
ninatatiza la fizi kutoka damu hasahasa ninapopiga au nikiyanyonya mate kwanguvu mswaki.
pia meno yangu yoote ya sebuleni (ya mbele) yanatikisika mmno kiasi siku nikijichanganya tu na kumchokoza bansa aka ni pa! mdomoni
yote naya tema.
yani yanatikisika mno kiasi hata nikitumia nguvu kungoa yanatoka.
halafu yanauma. nisaidieni jamani.
<br />Tarehe 08/02, nilimuona daktari akanipa appointment, aliniambia meno yangu yanahitajika kusafishwa. So tarehe 10/02, nilienda nikasafishwa meno. Kweli kulikuwa na uchafu mgumu uliokuwa umeganda kwenye meno ya chini, hivyo alifanikiwa kuutoa karibia wote. Akaniambia ninunue hydrogen peroxide (mouth wash) niwe naskutua asubuhi, mchana na jioni. Pia akaniambia nirudi baada ya wiki moja tuone kama meno yatakuwa yameanza kukaza. <br />
Kuanzia hapo tatizo la kutokwa damu limekata, ila meno bado yanaum( si mara kwa mara) halafu nahisi bado hayajakaza kama nilivyotarajia kwa haraka. Ngoja nitaendelea kuwapa feedback. Asanteni nyote
Si ndo itakuwa vizuri mzee unajipunguzia na matatizo ya kung'ang'ana na mifupa na vitu vigumu. Wewe utakuwa mtu wa softsoft tu, mayai, soda, nk!
Kama hukubaliani na ushauri huo basi kamwone dentist.