Kama issue ni rates tu mleta uzi utakuwa umewaonea Astra
Issue sio rates pekee. Hapa ni kutoa quoation kubwa zaidi na malipo yanayokwenda bima kuwa ni kidogo...yaani yale mambo ya 10%
gazeti linasema kuna cover ya afya ya 3billion lakini zika pigwa 6billion
kuhusu rates wana toza chini ya makubaliano ya industry. industy ya bima kupitia TIRA,TIBA na ATI Waliajiri actuarial valuation ili ashauri juu ya njia bora za kutoza pemium... hii ni kwa ajili ya kulinda soko la bima lisifilisike na kuweka minimum rates amabpo lengo ni kulinda ushindani.
sasa hii kampuni imekua ikikeuka haya na ku charge chini ya viwango...hivyo ni kinyume ya trade fair competition. ..
hili suala lina husu baadhi ya makampuni makubwa ya broker 10 yanayo ngoza kwa mapato
hawa kwa pamoja yana kusanya zaidi ya 80% ya mapato yote ya bima. ..amabayo ni wastani wa zaidi ya
400 bilion kwa mwaka.
sasa kutokana na ku rate chini ya nusu ya rates zilizo kubaliwa basi huikosesha serikali mapato ya VAT Zaidi ya
36 BILLION
kama wangefata rates zilizo kubaliwa basi wao pekee yao wangekusanya zaidi ya
600 Billion. lakini kutokana na uhuni wanao fanya ili kuhodhi biashara hiii basi serikali inakosa mapato yake . hii ni sawa Kununua TV ya 1Milion lakini mwenye duka anakuandikia risti ya laki 2 !!!
Tatizo hili lanafanya makampuni ya wazalendo washindwe kushindana na uhuni huu ..kwani always mteja atakwenda pale anapopata bi nafuu.
Tatizo lingine ni makampuni mengi ya bima kusajiliwa kijanja janja.
utakuta Watu wanaanzisha Broker then wakati huo huo wanahisa kubwa kwenye kampuni za bima zenyewe... sasa utakuta Mume ni MD wa Broker na Mke wake ni M. Director wa Insurance Company...sheria inaruhusu Broker kumiliki 10% interest katika Kmapuni za Bima lakini imekua ikitumiwa vibaya sana na baadhi ya Ma broker wakubwa Kujianzishia Makampuni ya Bima yao ili kuwa na total control ya market.
unaweza kukuta majina makubwa ya kampuni lakini local share holder ni Broker. sasa huku ndio wanapitishia kufanya under cutting na madudu mengine.
Hapa sheria ibadilishwe Brokers wasiruhusiwe kuwa na hisa kwenye makampuni ya Bima.
yapo mambo mengi yanaendelea katika hii secta na inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa...
Tutaendelea Kujuvyana zaidi kuhusu secta hii lengo likiwa kuona serikali inachuka hatua . Tukumbuke BIMA IMARA NDIO MLINZI WA UCHUMI WA NCHI...STAY TUNNED