Kampeni za Uchaguzi Mkuu ujao, nitawauliza wagombea urais ni hatua gani kali sana dhidi ya Watanzania wenzako unaweza kuchukua ili kuzima madai yao?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Nina hamu sana ya kuwauliza wagombea Urais wa vyama mbalimbali maswali haya chini ikiwa nitapata nafasi ya kushiriki kwenye mdaharo wa wagombea uraisi;

  1. Miaka kadhaa iliyopita, Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM alishauri Tanzania iingie kwenye mfumo wa vyama vingi japo ni asilimia 20% tu ya wananchi iliyomonyesha kutaka mfumo wa vyama vingi vya siasa. Je,katika kuwa raisi anaefuata demokrasia, wewe una maoni gani kuhusu ushauri wa Nyerere, alipindisha haki ya wengi? Wewe ungefanyaje katika hali ile?
  2. Ikitokea kwamba katika uongozi wako kama raisi wa kidemokrasia, asilimia labda 20 kama iliyotaka mfumo wa nyama vingi vya siasa, ina madai ya mabadiliko katika sheria za nchi na hata kutaka waandamane kuonyesha hisia zao kushinikiza mabadiliko, jambo ambalo ukaona ni tishio kwa chama chako cha siasa, utaona ni halali kutumia nguvu ya kiasi gani ili kunyamazisha kundi hilo;
    1. Nguvu isiyosababisha kifo cha Mtanzania hata mmoja ili kutotekeleza madai yo?
    2. Vipi ikiwa nguvu inaweza kusababisha vifo vya Watanzania zaidi ya 50, utaruhusu itumike badala ya kutekeleza madai yao?
    3. Vipi ikiwa nguvu inaweza kusababisha vifo vya Watanzania chini ya 20, utaruhusu itumike badala ya kutekeleza madai yao?
    4. Vipi ikiwa nguvu inaweza kusababisha vifo vya Watanzania chini ya 10, utaruhusu itumike badala ya kutekeleza madai yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…