Kama ni wewe ungefanya nini?

Mr mgeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,222
Reaction score
812
Pale utakapogundua kwamba,mkeo kakuzalia mtoto ambae si damu yako.


Utafanya nini,au utachukua maamuzi gani?
 
Lea tu, hiyo ni pilipili imeota kwenye shamba lako la mahindi
 
inategemea na ukweli umeupataje?

je? ni ripoti ya mkemia ama maneno ya majirani ama wasiwasi wako tu na kutofanana na mtoto.

kwa mimi namlea huyo mtoto alafu natia wangu mapema iwezekanavyo
 
Pole, yamekukuta? Lea mtoto mpaka ankatae baba yake mzazi!
Mimi nimewahi kulea mtoto wa shemeji yangu aliyezalishwa na mtoto kukataliwa na baba yake!
Sasa mimi ndiye ananitambua mtoto kama ndiye baba mzazi japo anajua ukweli kuwa sio baba yake mzazi!
Nimemsomesha na alipofika darasa la nne akakataa jina la baba yake shule akaomba atumie la kwangu!
Sasa anamaliza darasa la saba na hataki kumuona baba yake mzazi japo jamaa mara kadhaa anaomba msamaha!
Dogo hampendi baba yake hatari! Pia angalia diamond anavyomchukulia baba yake!
Lea maana hujui atakayekuzika!
Wala usiachane na mkeo kama nawe pia una watoto nae!
Ndo changamoto za ndoa hizo hasa wanawake waendeshwao na tamaa za miili yao!
Nakwambia mpende mtoto huyo na ndo dawa ya mkeo kukata tamaa ya mwili wake kwa wanaume wengine!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Yusufu alimlea mtoto asie wake- Yesu
 
Sawa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…