Samson Mwigamba
MARA nyingi namshukuru Mungu na ndiyo
maana mara kadhaa nimeandika kusema
Rais Kikwete alikuwa chaguo la Mungu na
CHADEMA ni mpango wa Mungu.
Kikwete ni chaguo la Mungu kwa kuwa
aliruhusu achaguliwe mtu aliyeonekana
maarufu kuliko wote ndani ya CCM, mtu
aliyeonekana makini kuliko wote ndani ya
CCM, mtu aliyeonekana jasiri kuliko wote
ndani ya chama hicho, mtu aliyeonekana
kama ni yeye tu aliyebaki ndani ya chama
anayeweza kulifanyia taifa hili mabadiliko
makubwa, kumbe zilikuwa ni ndoto za
mchana.
Amekwama kuliko marais wote
waliomtangulia! Lakini kwa nini Mungu
aliruhusu achaguliwe na kuwa rais wetu
kwa miaka 10? Lilikuwa ni chaguo lake.
Lilikuwa ni chaguo lake la kutekeleza
mpango wake kupitia CHADEMA.
Mungu aliiandaa CHADEMA kabla hata
chama hicho hakijaundwa ili kije
kumkomboa Mtanzania. Lakini kumshawishi
Mtanzania kwamba chama kingine ndicho
kitakacholeta ukombozi na mabadiliko ya
kweli katika nchi hii, ilikuwa ni vigumu kama
ilivyokuwa vigumu kumshawishi Myahudi
kwamba Yesu Kristo ndiye masihi aliyekuwa
anasubiliwa.
Ndipo Mungu akaona njia ya pekee ilikuwa
kumwinua Kikwete, kumpa umaarufu na
hatimaye aonekane ni yeye peke yake
aliyebaki ndani ya CCM na wampe kura
nyingi ambazo hazijawahi kutokea kwenye
uchaguzi wa vyama vingi hapa Tanzania
lakini aje aboronge kuliko wote na ndipo
Watanzania wataanza kuangalia nje ya CCM
na kuikuta CHADEMA ambayo itakuwa
tayari imeandaliwa na Mungu kama
inavyotokea hivi sasa.
Nilipoanza tu kuandika makala hizi
Septemba mwaka 2007, katika makala yangu ya kwanza kabisa (Septemba 19, 2007) niliandika juu ya unabii wa kuanguka kwa CCM utakavyotimia.
Ndani ya makala ile nilieleza kwamba:
Ndipo kuelekea mwishoni mwa utawala
huu, wananchi watapiga kelele. Baadhi ya
vyombo vya habari vilivyoupigia debe
utawala huu vitajiona viliwasaliti
Watanzania.
Vitaungana na vyombo vya habari makini
kupiga kelele itakayosikika kila kona ya nchi
kwamba uhuru wa kweli na mabadiliko ya
kweli bado yanahitajika.
Wanafunzi wa vyuo na sekondari watapaza
sauti, watumishi wa umma na binafsi
watapiga kelele kila kona wakiambiana:
Hakuna njia ya kuleta mabadiliko nchi hii
bila kuipiga chini CCM.
Baada ya chaguo la Mungu kushindwa
kuleta mabadiliko, sasa itakuwa ni dhahiri
kwamba hata malaika ndiye awe rais wa
Tanzania kupitia CCM kwa mfumo uliopo,
hakuna mabadiliko yoyote.
Kule vijijini, walimu wa shule za msingi na
sekondari watageuka na kuwa walimu wa
wananchi wa vijijini wasio na uelewa
mpana na mwamko wa mambo ya kisiasa.
Watawaelewesha kuwa mabalozi wa
nyumba kumi ni viongozi wa CCM tu, na
hawana haki wala uwezo wa kuwatisha
wananchi hata waichague CCM bila ridhaa
yao.
Watawaelimisha kwamba Tanzania
itaendelea kuwa nchi ya amani, tena amani
ya kweli (si ya uongo) bila CCM. Wala
anguko la CCM halitaifanya nchi iwe na vita
kama Rwanda na Burundi.
Watawaelimisha wananchi nao
watayapuuza madai hayo ya kutungwa na
CCM, wasiwe na wasiwasi maana chama
cha upinzani kikishinda majeshi yote yataitii
serikali mpya na kama CCM wana mpango
wa kushika silaha na kuingia msituni
watakamatwa hata kabla hawajafika ukumbi
wa Chimwaga kupanga mipango hiyo.
Kama kuna kitu huwa kinanipa imani na
ujasiri wa kusonga mbele ni jinsi baadhi ya
tabiri zangu na za waandishi wenzangu
kina Mwanakijiji, Kibanda, Ngurumo,
Malera, Mwalimu mkuu wa watu, Juvenalis
Ngowi, Saed Kubenea na wengineo wengi
zinavyotimia haraka.
Katika makala hiyo ya kwanza kwa mfano
nilizungumzia watumishi wa umma na wa
sekta binafsi kuungana kupiga vita dhidi ya
serikali ya chama kilichoko madarakani na
kudai mabadiliko. Sijui ni wangapi wanaona
utimilivu wa utabiri huo.
Wanaoangalia haraka haraka hawawezi
kuona jinsi watumishi wa umma na wale wa
binafsi wanavyopigania mabadiliko. Na hii
ni kwa sababu hawatoki majukwaani kama
sisi tulio viongozi wa chama.
Napenda leo makala yangu itoe shukrani za
pekee kwa watumishi hawa ambao
nimewaita malaika wasioonekana.
Nawasihi Wana CHADEMA wote viongozi,
wanachama wa kawaida, wapenzi,
mashabiki, na wapenda na/au wapigania
mabadiliko wote tuwashukuru hawa watu
kwa namna ya pekee sana!
Ngoja niwaambie kitu wasomaji wa Kalamu
hii: CHADEMA imefika hapo ilipo kwa
sababu ya bidii ya viongozi waanzilishi kina
mzee Mtei, marehemu Bob Makani, kina
Freeman Mbowe, kina Victor Kimesera, na
wengineo, kwa msaada wa sisi viongozi
wengine tuliojiunga baadaye na kushika
nafasi za uongozi sehemu mbalimbali na
katika ngazi mbalimbali.
Lakini CHADEMA kubaki hapo ilipo kuna
msaada wa tatu. Huu ni msaada wa malaika
wasioonekana. Malaika hawa kama
nilivyosema watumishi katika sekta ya
umma na binafsi (hapa najumuisha mpaka
waliojiajiri wenyewe).
Hawa wanaweza kuwa walimu wanaosaidia
kutoa elimu ya uraia kwa wanafunzi
wanaopita mikononi mwao na hata wazazi
na wananchi kwa ujumla. Pia wapo
watumishi katika vyombo vyetu vya usalama
wenye vyeo na wasiokuwa na vyeo ambao
kuna wakati wanafikia kusimama kidete
kwenye sheria zao za kazi na kukataa
kutumiwa na wanasiasa wasioipenda
CHADEMA.
Ndio wale aliowasema katibu mkuu wa
chama kwamba wanafikia kumletea taarifa
za mipango michafu dhidi ya chama.
Kuna watu kwenye vyombo vya habari
ambao nao wako macho kubaini maandishi
ya hila yanayolenga kuharibu taswira nzuri
ya chama kwa jamii.
Hawa wako tayari kuhatarisha wakati
mwingine vibarua vyao kwa kusimamia
ukweli na huzitumia vema kalamu zao na
midomo yao kukitetea chama. Siwezi
kuwasahau watumishi wa mabenki wale
waliofanya kazi nzuri kubaini na kuweka
wazi michoro ya jinsi pesa zilivyokuwa
zinatembea mabilioni kwa mabilioni kutoka
akaunti moja ya benki moja kwenda akaunti
nyingine ya benki nyingine ikiwa ni pamoja
na Benki Kuu.
Ni kwa msaada wao leo ufisadi wote EPA,
Deep Green Finance, Meremeta na
mwingineo, uko wazi kwa Watanzania.
Lakini kuna vijana wataalamu wa kompyuta
na IT ambao hawatumwi na mtu ila
likitokea jambo lenye mashaka dhidi ya
CHADEMA wao hutumia utaalamu wao
haraka kubaini mchezo uko wapi.
Nakumbuka kwa mfano wakati kina Slaa
wanalalamikia CCM kuingiza mtambo
unaoweza kutuma ujumbe wa simu kutoka
namba yoyote kwenda namba yoyote, watu
walikataa na hasa CCM wakidai hilo
haliwezekani. Lakini vijana hawa bila
kutumwa na mtu, haraka sana walifuatilia
na hatimaye kukaweka hako ka-software
kwenye mtandao wa kijamii ili Watanzania
wajue inawezekana na baada ya hapo
sijaisikia tena kesi ya Mwigulu Nchemba
dhidi ya Mnyika na meseji za vitisho.
Kuna vijana wako huko kwenye mitandao ya
simu. Usifanye uhuni kama ule aliofanya
Mwigulu na Ludovick ukadhani
hautajulikana. Vijana wataleta hadharani
mawasiliano yote na hutakuwa na mahali
pa kukwepea!
Nikiri kwamba watu hawa wako wengi
kwenye makundi mengi ambayo mengine
siwezi hata kuyajua. Labda niishie kwa hao
wawe wawakilishi na naamini baada ya
makala hii kusomwa, kuna wengine
watanijulisha makundi yao na wakipenda
nitayataja makundi yao kwenye makala
zijazo!
Lakini mimi nasema, ingekuwa nguvu ya
kina Slaa, Mbowe, Zitto na wengineo peke
yao, hiki chama kingekwisha kusambaratika,
maana ndilo wanalohangaika nalo
wapinzani wetu usiku na mchana.
Lakini kwa kazi inayofanywa na hawa
malaika wasioonekana ni kubwa mno.
Wakati mwingine sisi viongozi tumelala
fofofo usiku kumbe wapinzani wetu
hawajalala wanapanga mikakati na kuiingiza kazini.
Ni malaika hawa ambao nao hawalali
ambao hupambana na mbinu hizo na sisi
tunakuja kushangaa kuona mkakati
hadharani na jinsi ulivyozimwa!
Hawa nao wameandaliwa na Mungu ili
watumike kukamilisha mpango wake na kwa
kuwa wameikubali sauti ya Mungu na
wanatumika kwa moyo mmoja, bila malipo
wala bila kuombwa kufanya hivyo na mara
nyingi kwa sababu hatuwajui huwa hata
hatuwashukuru, leo naomba kwa niaba ya
viongozi wote wa CHADEMA katika ngazi
zote niwashukuru sana.
Na ni rai yangu kwamba viongozi wa chama
tujenge utaratibu wa kuwashukuru hawa
watu hata majukwaani ingawa wengine hata hatuwajui lakini naamini watajisikia furaha moyoni kwa kutambuliwa tu kazi yao.
Naamini rais wa kwanza kutoka CHADEMA
2015 atakapolihutubia taifa kwa mara ya
kwanza hatasahau kuwataja kwa jina lake
atakaloona linafaa, ingawa mimi
nimechagua kuwaita malaika
wasioonekana. Asanteni sana na mpango
wa Mungu utatimia hakika!
MARA nyingi namshukuru Mungu na ndiyo
maana mara kadhaa nimeandika kusema
Rais Kikwete alikuwa chaguo la Mungu na
CHADEMA ni mpango wa Mungu.
Kikwete ni chaguo la Mungu kwa kuwa
aliruhusu achaguliwe mtu aliyeonekana
maarufu kuliko wote ndani ya CCM, mtu
aliyeonekana makini kuliko wote ndani ya
CCM, mtu aliyeonekana jasiri kuliko wote
ndani ya chama hicho, mtu aliyeonekana
kama ni yeye tu aliyebaki ndani ya chama
anayeweza kulifanyia taifa hili mabadiliko
makubwa, kumbe zilikuwa ni ndoto za
mchana.
Amekwama kuliko marais wote
waliomtangulia! Lakini kwa nini Mungu
aliruhusu achaguliwe na kuwa rais wetu
kwa miaka 10? Lilikuwa ni chaguo lake.
Lilikuwa ni chaguo lake la kutekeleza
mpango wake kupitia CHADEMA.
Mungu aliiandaa CHADEMA kabla hata
chama hicho hakijaundwa ili kije
kumkomboa Mtanzania. Lakini kumshawishi
Mtanzania kwamba chama kingine ndicho
kitakacholeta ukombozi na mabadiliko ya
kweli katika nchi hii, ilikuwa ni vigumu kama
ilivyokuwa vigumu kumshawishi Myahudi
kwamba Yesu Kristo ndiye masihi aliyekuwa
anasubiliwa.
Ndipo Mungu akaona njia ya pekee ilikuwa
kumwinua Kikwete, kumpa umaarufu na
hatimaye aonekane ni yeye peke yake
aliyebaki ndani ya CCM na wampe kura
nyingi ambazo hazijawahi kutokea kwenye
uchaguzi wa vyama vingi hapa Tanzania
lakini aje aboronge kuliko wote na ndipo
Watanzania wataanza kuangalia nje ya CCM
na kuikuta CHADEMA ambayo itakuwa
tayari imeandaliwa na Mungu kama
inavyotokea hivi sasa.
Nilipoanza tu kuandika makala hizi
Septemba mwaka 2007, katika makala yangu ya kwanza kabisa (Septemba 19, 2007) niliandika juu ya unabii wa kuanguka kwa CCM utakavyotimia.
Ndani ya makala ile nilieleza kwamba:
Ndipo kuelekea mwishoni mwa utawala
huu, wananchi watapiga kelele. Baadhi ya
vyombo vya habari vilivyoupigia debe
utawala huu vitajiona viliwasaliti
Watanzania.
Vitaungana na vyombo vya habari makini
kupiga kelele itakayosikika kila kona ya nchi
kwamba uhuru wa kweli na mabadiliko ya
kweli bado yanahitajika.
Wanafunzi wa vyuo na sekondari watapaza
sauti, watumishi wa umma na binafsi
watapiga kelele kila kona wakiambiana:
Hakuna njia ya kuleta mabadiliko nchi hii
bila kuipiga chini CCM.
Baada ya chaguo la Mungu kushindwa
kuleta mabadiliko, sasa itakuwa ni dhahiri
kwamba hata malaika ndiye awe rais wa
Tanzania kupitia CCM kwa mfumo uliopo,
hakuna mabadiliko yoyote.
Kule vijijini, walimu wa shule za msingi na
sekondari watageuka na kuwa walimu wa
wananchi wa vijijini wasio na uelewa
mpana na mwamko wa mambo ya kisiasa.
Watawaelewesha kuwa mabalozi wa
nyumba kumi ni viongozi wa CCM tu, na
hawana haki wala uwezo wa kuwatisha
wananchi hata waichague CCM bila ridhaa
yao.
Watawaelimisha kwamba Tanzania
itaendelea kuwa nchi ya amani, tena amani
ya kweli (si ya uongo) bila CCM. Wala
anguko la CCM halitaifanya nchi iwe na vita
kama Rwanda na Burundi.
Watawaelimisha wananchi nao
watayapuuza madai hayo ya kutungwa na
CCM, wasiwe na wasiwasi maana chama
cha upinzani kikishinda majeshi yote yataitii
serikali mpya na kama CCM wana mpango
wa kushika silaha na kuingia msituni
watakamatwa hata kabla hawajafika ukumbi
wa Chimwaga kupanga mipango hiyo.
Kama kuna kitu huwa kinanipa imani na
ujasiri wa kusonga mbele ni jinsi baadhi ya
tabiri zangu na za waandishi wenzangu
kina Mwanakijiji, Kibanda, Ngurumo,
Malera, Mwalimu mkuu wa watu, Juvenalis
Ngowi, Saed Kubenea na wengineo wengi
zinavyotimia haraka.
Katika makala hiyo ya kwanza kwa mfano
nilizungumzia watumishi wa umma na wa
sekta binafsi kuungana kupiga vita dhidi ya
serikali ya chama kilichoko madarakani na
kudai mabadiliko. Sijui ni wangapi wanaona
utimilivu wa utabiri huo.
Wanaoangalia haraka haraka hawawezi
kuona jinsi watumishi wa umma na wale wa
binafsi wanavyopigania mabadiliko. Na hii
ni kwa sababu hawatoki majukwaani kama
sisi tulio viongozi wa chama.
Napenda leo makala yangu itoe shukrani za
pekee kwa watumishi hawa ambao
nimewaita malaika wasioonekana.
Nawasihi Wana CHADEMA wote viongozi,
wanachama wa kawaida, wapenzi,
mashabiki, na wapenda na/au wapigania
mabadiliko wote tuwashukuru hawa watu
kwa namna ya pekee sana!
Ngoja niwaambie kitu wasomaji wa Kalamu
hii: CHADEMA imefika hapo ilipo kwa
sababu ya bidii ya viongozi waanzilishi kina
mzee Mtei, marehemu Bob Makani, kina
Freeman Mbowe, kina Victor Kimesera, na
wengineo, kwa msaada wa sisi viongozi
wengine tuliojiunga baadaye na kushika
nafasi za uongozi sehemu mbalimbali na
katika ngazi mbalimbali.
Lakini CHADEMA kubaki hapo ilipo kuna
msaada wa tatu. Huu ni msaada wa malaika
wasioonekana. Malaika hawa kama
nilivyosema watumishi katika sekta ya
umma na binafsi (hapa najumuisha mpaka
waliojiajiri wenyewe).
Hawa wanaweza kuwa walimu wanaosaidia
kutoa elimu ya uraia kwa wanafunzi
wanaopita mikononi mwao na hata wazazi
na wananchi kwa ujumla. Pia wapo
watumishi katika vyombo vyetu vya usalama
wenye vyeo na wasiokuwa na vyeo ambao
kuna wakati wanafikia kusimama kidete
kwenye sheria zao za kazi na kukataa
kutumiwa na wanasiasa wasioipenda
CHADEMA.
Ndio wale aliowasema katibu mkuu wa
chama kwamba wanafikia kumletea taarifa
za mipango michafu dhidi ya chama.
Kuna watu kwenye vyombo vya habari
ambao nao wako macho kubaini maandishi
ya hila yanayolenga kuharibu taswira nzuri
ya chama kwa jamii.
Hawa wako tayari kuhatarisha wakati
mwingine vibarua vyao kwa kusimamia
ukweli na huzitumia vema kalamu zao na
midomo yao kukitetea chama. Siwezi
kuwasahau watumishi wa mabenki wale
waliofanya kazi nzuri kubaini na kuweka
wazi michoro ya jinsi pesa zilivyokuwa
zinatembea mabilioni kwa mabilioni kutoka
akaunti moja ya benki moja kwenda akaunti
nyingine ya benki nyingine ikiwa ni pamoja
na Benki Kuu.
Ni kwa msaada wao leo ufisadi wote EPA,
Deep Green Finance, Meremeta na
mwingineo, uko wazi kwa Watanzania.
Lakini kuna vijana wataalamu wa kompyuta
na IT ambao hawatumwi na mtu ila
likitokea jambo lenye mashaka dhidi ya
CHADEMA wao hutumia utaalamu wao
haraka kubaini mchezo uko wapi.
Nakumbuka kwa mfano wakati kina Slaa
wanalalamikia CCM kuingiza mtambo
unaoweza kutuma ujumbe wa simu kutoka
namba yoyote kwenda namba yoyote, watu
walikataa na hasa CCM wakidai hilo
haliwezekani. Lakini vijana hawa bila
kutumwa na mtu, haraka sana walifuatilia
na hatimaye kukaweka hako ka-software
kwenye mtandao wa kijamii ili Watanzania
wajue inawezekana na baada ya hapo
sijaisikia tena kesi ya Mwigulu Nchemba
dhidi ya Mnyika na meseji za vitisho.
Kuna vijana wako huko kwenye mitandao ya
simu. Usifanye uhuni kama ule aliofanya
Mwigulu na Ludovick ukadhani
hautajulikana. Vijana wataleta hadharani
mawasiliano yote na hutakuwa na mahali
pa kukwepea!
Nikiri kwamba watu hawa wako wengi
kwenye makundi mengi ambayo mengine
siwezi hata kuyajua. Labda niishie kwa hao
wawe wawakilishi na naamini baada ya
makala hii kusomwa, kuna wengine
watanijulisha makundi yao na wakipenda
nitayataja makundi yao kwenye makala
zijazo!
Lakini mimi nasema, ingekuwa nguvu ya
kina Slaa, Mbowe, Zitto na wengineo peke
yao, hiki chama kingekwisha kusambaratika,
maana ndilo wanalohangaika nalo
wapinzani wetu usiku na mchana.
Lakini kwa kazi inayofanywa na hawa
malaika wasioonekana ni kubwa mno.
Wakati mwingine sisi viongozi tumelala
fofofo usiku kumbe wapinzani wetu
hawajalala wanapanga mikakati na kuiingiza kazini.
Ni malaika hawa ambao nao hawalali
ambao hupambana na mbinu hizo na sisi
tunakuja kushangaa kuona mkakati
hadharani na jinsi ulivyozimwa!
Hawa nao wameandaliwa na Mungu ili
watumike kukamilisha mpango wake na kwa
kuwa wameikubali sauti ya Mungu na
wanatumika kwa moyo mmoja, bila malipo
wala bila kuombwa kufanya hivyo na mara
nyingi kwa sababu hatuwajui huwa hata
hatuwashukuru, leo naomba kwa niaba ya
viongozi wote wa CHADEMA katika ngazi
zote niwashukuru sana.
Na ni rai yangu kwamba viongozi wa chama
tujenge utaratibu wa kuwashukuru hawa
watu hata majukwaani ingawa wengine hata hatuwajui lakini naamini watajisikia furaha moyoni kwa kutambuliwa tu kazi yao.
Naamini rais wa kwanza kutoka CHADEMA
2015 atakapolihutubia taifa kwa mara ya
kwanza hatasahau kuwataja kwa jina lake
atakaloona linafaa, ingawa mimi
nimechagua kuwaita malaika
wasioonekana. Asanteni sana na mpango
wa Mungu utatimia hakika!