Whatever, vyovyote hebu sepa kama haijakuuma mbona unajibu. Nipotezee kwenye threads ninazoweka. Uliuchuna ila ilikupata ndo maana ukaja kujibu hapa.
Najibu hapa ili kutokuchafua Hali ya Hewa pande zile, na sitoweza kuchafua Hali ya Hewa pande zile hata Siku moja.
Busara ni kitu Muhimu sana MALAIKA wewe nakuambia.
Mimi sitoweza kukupotezea Mtoto Mzuri kama wewe.
Nakupa sababu chache tu ambazo sitoweza kukupotezea.
Mojawapo, Mimi nachangia ile Mada ninayojisikia kuchangia bila kujali nani aliebandika Mada husika. Kwasababu sina matatizo na Mtu, na sitimbi pande hizi za JF kihisia. Mimi natia Maguu humu kwa ajili ya kubadilishana Mawazo, Kutaniana, Kuwekana sawa, Kuelimishana, Kufunzana (sababu mimi napenda sana kujifunza mambo mapya), na mengine mengi sana ambayo sitoweza kuyaorodhesha yote, na Ndugu zangu wapendwa bila kujali Rangi zao, Imani zao, ikiwemo na wewe mwenyewe.
Huwa sina mambo ya Vikundi, mimi huwa najichanganya vile ninavyojisikia kwasababu Mimi ni Mtu wa kujiachia. Na ndiyo Hali halisi ya Maisha yangu ninayoishi.
Kwahiyo nakushangaa sana unaposema nikupotezee, hicho hakitotokea hata siku moja. Nitakapoweza Mimi kukupotezea wewe ni pale utakapoanzisha mfano Blogu yako, hapo sawa. Sababu sitokuwa na Muda wa kuitembelea.
Lakini hapa JF!
Hayo ni masikhara ya hali ya juu. Huwezi kunipangia wapi nichangie, na wapi nisichangie.
Kingine, Mimi sitoweza kukupotezea wewe sababu kuna msaada mkubwa (si wa Kipesa) unahitaji kutoka kwangu, na mimi nitakuwa na wewe Bega kwa Bega.
Kwanini nasema unahitaji msaada mkubwa kutoka kwangu?
Jibu ni kwamba, kunishambulia kwako bila ya sababu kumenifanya Nikupende ghafla (sio Kimalavi Davi).
Kuna kitu kimoja kimekuanika sema wewe mwenyewe hufahamu, sababu huna uwezo wa kufahamu nilichokifahamu Mimi.
Na sitokitaja kwasababu zangu Maalum.
Kwa kumalizia, kama ukishindwa hapa naomba hata uninong'oneze. Yaani poa tu, haina noma wala nini sababu Mimi ni Mtu wa kuelewa sana.
Nimejisahau, nilitaka kumwaga Mtama kwenye Kuku wengi, haina haja ngoja nikaushe.
Mimi nakutakia Kila la kheri katika Maisha yako ya kila Siku, na Mungu Mwema akufanyie wepesi kwa kila jambo lako.
Ubarikiwe sana