Juma Matokeo (marehemu), Mid-field Maestro

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707

Alikuwa anachezea yanga miaka ya 1975-80 akitokea Tumbaku yaMorogoro,sijaona mchezaji mahili kama yeye , hajawahi kutokea, alikuwa na dribblingza kipekee , alikuwa anapendeza kumwangalia. Ile mechi ya club bingwa Africa mwaka1975 kati ya Yanga na Enugu rangers Juma Matokeo alikuwa man of the match mzeeTenga alipiga no 4.

Bongo zamani mpira ulikuwepo siyo sasa wachezaji wetuwanacheza gombe sugu.
 
Apumzike kwa amani, namkumbuka kama kocha wangu pale Makongo Sekondari miaka ile
 
Juma Matokeo ninayemkumbuka mimi ni enzi akiwa Pan Africa hii: Juma Pondamali, Mohammed Mkweche, Juma Matokeo, Leodgar Tenga, Jellah Mtagwa, Mohammed Rishard 'Adolf', Goldian Mapango, Mohammed Yahya 'Tostao', Ali Katolilah Peter Tino, na Ibrahim Kiswabi.

Vv
 
nakikumbuka hiki kikosi Forward ilikuwa na watu walioshiba na wenye mashuti makali
 
nakikumbuka hiki kikosi Forward ilikuwa na watu walioshiba na wenye mashuti makali

Kwenye kile kikosi mwenye umbo dogo na mfupi alikuwa Goldian Mapango pekee, lkn Tostao alikuwa kitu lililoshiba, Peter Tino, Ali Katollila, Jella Mtagwa, na Ibrahim Kiswabi walikuwa mapandikizi ya watu.

Kiswabi, alikuwa na umbo la kawaida si kama hawa wengine, Actually mmemsahau Abdallah Burhani, huyu ilikuwa habari nyingine. Njemba ilikuwa imeshiba hasa hasa
 
Mzee mwenzangu humu dotcom wengi ni kama unampigia mbuzi gitaa.
 
Kiswabi, alikuwa na umbo la kawaida si kama hawa wengine, Actually mmemsahau Abdallah Burhani, huyu ilikuwa habari nyingine. Njemba ilikuwa imeshiba hasa hasa

Huyo Burhani alikuja baadaye kidogo na unanikunbusha Pan Africa iliyopambana na Power Dynamo ya Zambia ktk Kombe la Washindi miaka hiyo. Kiswabi alikuwa na umbo la kawaida kama Tenga, Adolf Rishard, Juma Matokeo na Pondamali. Ila mwenye umbo dogo kuliko wote alikuwa Goldian Mapango.

Soka na Muziki wa dansi ndizo nilikuwa burdan Kuu enzi hizo pamoja na sinema ktk zile kumi za New Chox, Avalon, Empire, Empress, Odeon, na Drive inn.

Vv
 
Halafu huyo Abdallah Burhan na Makumbi Juma ndio waliokuwa wanaunda striking force ya Pamba FC ya Kigoma, na langoni alisimama Juma Yusu (Juma Y) ambaye alijiunga na Pamba FC wakati Makumbi Juma Bongabonga akienda Yanga, na Abdalla Burundi (Abdallah Burhani) akienda Pan Africa.

Vv
 
Abdalaah Burhani, alikuja Pan, akitokea RTC Kagera, baada ya kucheza vizuri saana Challenge yeye akicheza 9, na Zamoyoni Mogela akicheza 10.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…