Nadhani useme unataka kitu gani? kwani haujui kuwa JK yuko Ikulu na kwa sasa anapumzika Mbugani amechoka kufanya shughuli za kuwaletea Watanzania Maendeleo?Sema staright forward kipi kifanyike kwani ukishajua alipo ndo hayo matatizo uliyoyalist japo kwa uchache yataisha? kwa mfano, hapo ulipo umeanza hata harakati za kuhakikisha CCM hairejei madarakani kwa kuanza tu kuwashawishi vijana, wazee na marafiki zako kwa hoja za msingi au unasubiri hadi tarehe za kampeni zitangazwe? Je, una kadi ya CDM (manake vingine ni vipandikizi vya CCM)?
Nadhani hatuhitaji kujua JK alipo, tunahitaji kuanza kupambana na CCM kuanzia sasa, muda umeisha na Watanzania tumezubaa muda mrefu watu wanakufa kwa umaskini unaosababishwa na viongozi wetu ambao vichwa vyao vimejaa MAJI badala ya Ubongo. Viongozi wanaofikiria "mimi" badala ya "sisi".
Nawasilisha.
ni dhambi kubwa sana kutumia matatizo ya wananchi kama daraja kufanya ushawishi wa kisiasa.kikwete yupo anashirikiana na watendaji wake kuwahudumia watanzania wote ukiwamo wewe unaeandika uzushi hapa.sukari ni tatizo ktk nchi za afrika mash.kenya inauzwa ef4400
uganda 5000.serikali inashirikiana na wadau kuwasaidia waathirika wa mafuriko nyie majina kapuni mnaenda kuiba ili ionekane govt imeshindwa kusimamia.tunazo tarifa zenu.acheni uchochezi.
JK aliingia madarakani kwa mbwembwe sana na ahadi lukuki na akiwa amebeba matumaini makubwa ya WaTZ. Tatizo yote ameyatelekeza na kuwaacha wananchi wakiwa hawana kimbilio wala pa kusemea. WaTZ kuandamana sio asili yetu ila unapoona tunaweza kuandamana, machinga wanapigana na mgambo na polisi, kule Mbeya juzi tu watu wanarushiwa mabomu ya machozi na wao wanayadaka na kuwarushia polisi,JUA KUWA TUMEPOTEZA TUMAINI NA NCHI YETU NA UTAWALA WAKE.
-Nchi inayolima miwa kibao inakuwa na uhaba wa sukari, tunanunua kilo kwa shs 3000 kama enzi zile za NMC kununua kwa mstari tena unaambiwa usinunue zaidi ya kilo 2.,
-watu wanagoma kuuza mafuta wananchi wanateseka nchi nzima na serikali imekaa kimya tu,
-watu wanaiba hela za serikali (EPA) na wanashauriwa warudishe then wanaendelea kufaidi maisha na serikali ipo tu
-Madini yanabebwa bure na wananchi wanaachiwa maji yenye madhara kwa afya zao na serikali inatabasam tu
-Watu wanaingia mikataba ya hovyo kama richmond na gharama zake anabebeshwa mwananchi
-Maisha ya mTZ yanazidi kushuka thamani kila siku
-Hospitali mtu anaenda kujifungua anaambiwa aende na pamba na gloves
-shule za msingi madawati hamna, walimu hamna, vitabu na vitendea kazi vingine hamna
-Vyuoni mikopo wanapewa watoto wa wakubwa na makabwela wananyimwa, migomo kila siku na ukigoma unafukuzwa
-Wahitimu kibao mtaani ajira hamna
-Serikali inanunua ma V8 ya 200mil. lakini bado inaongoza kuomba misaada nje na mikopo kila siku
-Walimu wanaidai serikali malimbikizo miaka nenda rudi lakini yenyewe inaandaa sherehe za uhuru wa miaka 50 wa nchi ambayo haipo (Tanganyika) kwa kila wizara- wengine wanahama toka dar kwenda kufanyia butiama
-Mishahara midogo kwa watumishi wa serikali na binafsi
-Uwekezaji ambao unawanufaisha wageni tu, waTZ wananyanyaswa kwenye migodi na makampuni ya wageni ya ujenzi lakini hawana pa kusemea maana serikali na vyama vya kuwatetea vimeshatiwa mfukoni na wawekezaji
-SERIKALI HATA KUWASAIDIA WALIOPATWA NA MAFURIKO DAR IMESHINDWA, CHA AJABU HATA MISAADA INAYOTOLEWA NA WASAMARIA WEMA WANASHINDWA KUILINDA NA INAIBIWA
Nauliza JK yuko wapi?