Kwanza nafurahi kuona kwenye rekodi kwamba kuna watu walilisema hili hata kabla ya mkutano wa IMF, kwa hiyo JK siyo tu hakujua cha kufanya, bali pia hakuwa akifuatilia magazeti ya nchini -seuze ya nje- yanasemaje.
JK alishatoa msimamo kwamba hatufanyi chochote tofauti, sasa mnataka msimamo gani tena?
Kama hukubaliani na msimamo huo onyesha mapungufu yake na mwaga pointi zako.Ukitoa hapo alipobofya na ku "cut and paste" kutoka Kenya, muandishi hajatuonyesha idea, achilia mbali idea original.
Ingawa nakubali kwamba kutoa policy si kazi ya muandishi, ningefikiri kuwa mtu mwenye kutoridhika kwa kiwango hiki, hususan muandishi wa siku nyingi kama bwana Bwire, angekuwwa na maoni yanayoweza kuleta mipango itakayotekelezeka. Ni rahisi kuona chombo kinaenda harijojo, hilo hata watoto wa shule za upili wenye akili wanaliona, kitu ambacho si rahisi kukijua ni jibu la swali, je tufanye nini?
This article is the personification of a wasted opportunity to raise a number of alternatives to combat the prevalent crisis.