Shukrani mkuu kwa darsa murua.
Nilipokua mdogo nilisumbuliwa sana na asthma, ilisababisha hata utoto wangu nisiu-enjoy vizuri kwa michezo mbalimbali hasahasa mpira na michezo ya kukimbizana. Nilihangaika sana na dawa za hospitali na kuna kipindi niliwahi kutumia hadi zile "inhalers".
Nilipofika darasa la 5 mzee wangu alipata bahati akakutana na mama mmoja hivi mmasai akaamua kunisaidia baada ya mzee kumsimulia tabu anayoipata kwa kunitibia.
Nilitumia asali, nilichanganya na unga fulani hivi (sikuwahi kujua unaitwaje) ila ulikua ni mchungu sana, pia kulikuwa na dawa nyingine ya kuweka kwenye chai ila ilikuwa inaniwasha sana kwenye koo, na pia kuna moja nilikuwa naitumia kwenye maji yenye mvuke na kuipitishia puani.
Mungu si athumani, hata sikumbuki nilipona lini ila mpaka nilipofika darasa la 6 nikajikuta naanza kucheza mpira, naoga maji ya baridi (wakati huo nilikuwa nikiishi mbeya na baridi ya kule si mchezo), natumia perfumes & sprays hadi leo hii na kufanya vitu vyote ambavyo sikuvitumia hapo kabla.[/Q