nimekusoma nikahisi labda hujaona heruf yako..... kumbe iko namna hii ndo maana ukasema wizi mtupu,,,,ha hahahhaha....
>HERUFI X
>Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.
Basi ukhti Nilham mimi nitaanza na ayah hii kutoka kwenye Qur'an:
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Q 005:90
Ukhti Nilham bint Rashed, unajuwa kuwa akili ing'aayo ni chemchemi neemevu inayomwendeleza mtu mbele zaidi kuliko mahitaji ya kidunia na inamjulisha ulimwengu mwingine pia. Fikra nzito na aali humzuia mwerevu asidanganyike na ulimwengu. Yule aliyekikuza na kukiimarisha kipaji chake cha fikra (akili) na akakifanya kuwa ni kitovu cha uvutano katika maisha yake, atakapofikwa na matukio machungu na mabaya, atachukua hatua inayofaa ya kifikra badala ya kuyakabili vibaya, na atabaki imara kamajabali. Na si kukimbilia wapiga ramli na watazamao nyota ili kupata ufumbuzi wa matatizo yao, kwani kufanya hivyo ni shirki kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Ili tujitoe katika mazingira ya fazaa na jahazi la uhai wetu lisikumbwe na mawimbi makubwa na madogo, ni lazima tuzidhibiti fikra zetu mpaka tafakuri sahihi zishike uongozi wetu, na nguvu zetu zote za kiroho ziweze kujizatiti na kusimama dhidi ya vitu vinavyoleta madhara na vinavyosababisha wasiwasi katika maisha yetu, yakiwemo haya ya kutazamia ramli na upigaji bao.
Uislamu kwa kutia nishati ya imani katika nyoyo za wafuasi wake, huhimiza na huimarisha msingi wa kudhaniana vizuri na kuaminiana kati ya watu; na kwa njia hiyo huuelekeza mwendo wa jamii katika mazingira yanayofaa na yaliyojaa itibari na utulivu.
Ni wajibu kwa kila Mwislamu amdhanie vizuri Mwislamu mwenzake, na aitazame amali ya mwenzake kwa njia sahihi na ya kisheria. Haruhusiwi mtu yeyote kuchukulia kitendo fulani cha Mwislamu kuwa ni kibaya na cha kifisadi kama hana ushahidi madhubuti na wa dhahiri, Basi ni hayo tu ukhti bint ami... Utanisamehe kama nitakuwa nimekukwaza.