Jionee ubora wa parachichi katika mwili wako

verykeys

Senior Member
Mar 29, 2016
155
90
Hili ni tunda lenye virutubisho vingi na muhimu kwa afya zetu, na inaelezwa kuwa tunda hili huenda likawa ni mbadala wa vyakula vya nyama kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake.

Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni.

Tunda hili pia husaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sambamba na kujenga neva na

Tunda hili pia huweza kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu na kusheheni vitamin A, B, C na E.

vyakula kama nyama husababisha 'uric acid' nyingi mwilini, ambayo husababisha magonjwa mengi mwilini, hivyo tunda hili huweza kusafisha hiyo na kuitoa nje na kuondoa magonjwa pia.

“Tunda hili hufanya vizuri sana kwa magonjwa hayo na kuyamaliza, lakini pia husaidia wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi,” alisema mtaalam huyo.

Pia majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu kunywa husaidia kuondoa matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo, kuumwa kichwa, koo (throat), tumbo, mapafu na uvimbe.

Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.

Pamoja na hayo parachichi huweza kutumika hata katika masuala ya urembo, ambayo ni pamoja na kukuza nywele na kuokoa wale wenye tatizo la nywele zinazoanguka.
 
avocados-620x400-noexp.jpg
 
Mkuu vipi kuhusu nguvu za kiume? Kuna sehem nilisoma,wanasema hili tunda linaongeza hizo nguvu,ni kweli?
 
Mkuu vipi kuhusu nguvu za kiume? Kuna sehem nilisoma,wanasema hili tunda linaongeza hizo nguvu,ni kweli?
Ni kweli inasaidia ila sio nguvu moja kwa moja. Inachosaidia ni kusafisha na kuongeza blood pressure inayosababisha bwana mkunaji kuwa na uwezo wa kuwa active kwa muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom