Chadema acheni kulialia bila kufahamu ni kwa nini mpaka wafanyakazi waliopigika nao pia wanashirikiana na CCM kuwagandamiza!!
Mfano walimu wa mkoa wa DSM wanaonekana kuikubali sana CCM na kaka mkuu wa Mkoa huo kwa sababu tu ya kupewa vitambulisho vya kusafiri bure kwenye Daladala.
Sasa Mapolisi nao sasa wanaonekana kuunga juhudi kutokana na kutojua sera za wapinzani hasa Chadema juu ya hatima ya vyeo vyao hasa wale wa juu ambao wanaonekana kupigania nafasi zao zinazotokana na Mamlaka ya Amiri jeshi mkuu ambaye anawanyima maslahi mazuri lakini anawasifu na kuwatukuza kwa kuwapa Uhuru wa kuwanyoosha wapinzani na wahalifu.
Chadema mlipaswa mjue kuwa watu pekee waliobakia kuwaunga mkoni ni wafanyakazi wa ngazi za chini wanaoishi kama kuku wa kienyeji mana mishahara yao haitoshi kuanzisha Foundation kama zile za Kutulia na Akina Magwangala ambazo zinatoa mapesa kwa wapigakura wanyonge.
Adui wa wapinzani sio Jeshi la Polisi bali katiba na sheria za Kikoloni zinazowafanya wakuu wa mikoa na mawaziri ambao ni makada wa CCM kuwa na mamlaka juu ya makamanda wa Polisi na hata majeshi mengine.
Wakubwa wa vyombo vya dola chini ya katiba na sheria hizi za wakoloni haziwezi kumpa nafasi kiongozi Mwadilifu yeyote ndani ya vyombo vya dola kama hataki kutumikia chama cha wenye madaraka. Hata kama ni mchapakazi na mwadilifu kiasi gani inabidi ajipendekeze na hata kuwanyanyasa binadama na ndugu zake waliopo upinzani ili kulinda madaraka yake yanayompa nafasi ya kutumbua mijihela kama wale waliohongwa mil 700 na kutaka kutorosha madini.
Hatujui michezo kama ile inafanyika kwa kiwango gani na nani hasa anairatibu. Wanaofanya hayo ni wazi kuwa wanajiamini kuwa ni sehemu ya kuwabeba Makada wa chama.
Kuna nchi moja kule America ya kusini mkuu mmoja wa vyombo vya ulinzi na usalama alikataa kushiriki wizi wa kura na kupindua matokeo kubeba chama Tawala ; alipohojiwa kwa nini anakataa kushiriki dhambi ya dhulma akajibu kwamba vyama vyote na wagombea wote ni wananchi wa nchi hiyo na wote walipewa nafasi sawa za kupiga kampeni kwa hiyo hawezi kumpendelea yeyote kwani itakua ni kinyume cha kiapo chake cha kutenda haki; kilichotokea ni watawala na chama chao kumtumia mkuu wa tume kufuta matokeo.
Baadae watawala wakashinda tena na wakamua kumsimamisha kazi yule mkubwa wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa madai kuwa ni mwanachama wa chama kikuu cha upinzani ,hivyo amekiuka katiba.
Alistaafishwa baada ya ushahidi kukosekana.
Chaajabu hakuna hata mbunge au kiongozi wa upinzani ndani ya nchi ile aliyewahi kumsemea popote yule muhanga wa kusimamia haki kwenye katikati ya mifumo ya dhulma ya kimadaraka.
Hili ndilo linalowafanya majeshi hasa wakubwa wao ambao wanapata maslahi mazuri na heshima kubwa kuamua kushirikiana na chama chenye kuwaweka kwenye fursa nzuri na kuwavurumisha mbali wapinzani wasioeleweka kuwa wamesimamia wapi juu ya kuendelea kubeba maslahi yao japo.
Tukirudi nchi za Afrika pia kuna tatizo sana kati ya vyama vya upinzani na vyombo vya dola.
Wapinzani wanacheza ngoma ya vyama tawala inayopigwa kwa kutumia majeshi kwa maana kuwa wapinzani wanatumia muda mwingi kulalamikia mfano Polisi bila kufanya utafiti na kujua shida zao na changamoto zao kisha kuja na Sera nzuri ya kuwakomboa, badala yake utasikia kuwa tukiingia madarakani tutalifuta jeshi la Polisi. Nani atakuruhusu uingie madarakani ili ukafute ajira yake?
Sent using
Jamii Forums mobile app