Jinsi Polisi wanavyotumika kuidhoofisha chadema Arusha

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
548
1,000
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Arusha,kimelalamika kuhujumiwa na chama cha mapinduzi(CCM) kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapa ili kukihujumu chama hicho katika maandalizi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akiongea na vyombo vya habari Katibu wa chadema wilayani humo,Innosent Kisanyage,amesema kuwa kwa sasa chama hicho kipo kwenye zoezi la uhakiki wa wanachama wake katika kata zote za jiji la Arusha,hivyo chama cha mapinduzi kinalitumia jeshi la polisi kuwakamata viongozi wake wa mitaa kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali.

Amefafanua kuwa wiki iliyopita katika kata ya Elerai viongozi wa chadema walivamiwa na polisi waliokuwa wameambatana na baadhi ya viongozi wa ccm,wakati viongozi hao wa chadema wakiendelea na zoezi la kuhakiki wa wanachama katika kata hiyo ili kujiandaa na uchaguzi ujazo.

‘’Chadema ni chama cha kisiasa chenye usajili halali lakini viongozi wake wamekuwa wakifanyiwa hujuma kwa lengo la kukidhoofisha kwa kuwakamata viongozi wake wakiwemo wanachama wakati wakitekeleza majukumu yao’’alisema Kisanyage.

Amelitaka jeshi la polisi kushughulika na masuala ya ulinzi wa raia na mali zao na kuacha kutumika kukibeba chama cha mapinduzi kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuminya demokrasia na uhuru wa wananchi kujieleza na kuchagua chama wakitakacho.

Naye diwani wa chadema katika kata ya Eleray ,Jofrey Kalumuna alisema chama cha mapinmduzi kinafanya hujuma za wazi kwa kulishirikisha jeshi la polisi jijini hapa kuhakikisha kuwa chadema inashindwa kufanya shughuli zake .

Alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi yake na kujiweka kando na masuala ya kisiasa kwani zoezi linaloendelea kwa sasa ni kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitalii ,alisema kinachofanywa na ccm ni uoga wa kushiriki uchaguzi huo ndio maana wanatumia mabavu kukidhoofisha chama cha chadema.

Kwa upande wake diwani wa viti maalumu chadema jijini hapa,Hapyness Chale amekitaka chama cha mapinduzi mkoani hapa kuacha kudeka na kushindwa kujiamini kwa kutegemea vyombo vya dola katika kujiendesha badala yake wawatumikie wananchi na kuwaletea maendeleo ili kukupenda chama hicho.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa,Longinus Tibishumbwamu alisema atalitolea ufafanuzi suala hilo kwa kuwa yupo kwenye kikao cha mkuu wa mkoa wa ArushaSent using Jamii Forums mobile app
 

hugo jr

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
286
500
hii nchi kwa sasa imeharibiwa kabisa, na jambo hili sio Arusha tu bali nchi nzima, Mungu atusaidie wa tz tupate viongozi wenye busara na wanaojali demokrasia
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,771
2,000
Chadema acheni kulialia bila kufahamu ni kwa nini mpaka wafanyakazi waliopigika nao pia wanashirikiana na CCM kuwagandamiza!!

Mfano walimu wa mkoa wa DSM wanaonekana kuikubali sana CCM na kaka mkuu wa Mkoa huo kwa sababu tu ya kupewa vitambulisho vya kusafiri bure kwenye Daladala.
Sasa Mapolisi nao sasa wanaonekana kuunga juhudi kutokana na kutojua sera za wapinzani hasa Chadema juu ya hatima ya vyeo vyao hasa wale wa juu ambao wanaonekana kupigania nafasi zao zinazotokana na Mamlaka ya Amiri jeshi mkuu ambaye anawanyima maslahi mazuri lakini anawasifu na kuwatukuza kwa kuwapa Uhuru wa kuwanyoosha wapinzani na wahalifu.

Chadema mlipaswa mjue kuwa watu pekee waliobakia kuwaunga mkoni ni wafanyakazi wa ngazi za chini wanaoishi kama kuku wa kienyeji mana mishahara yao haitoshi kuanzisha Foundation kama zile za Kutulia na Akina Magwangala ambazo zinatoa mapesa kwa wapigakura wanyonge.

Adui wa wapinzani sio Jeshi la Polisi bali katiba na sheria za Kikoloni zinazowafanya wakuu wa mikoa na mawaziri ambao ni makada wa CCM kuwa na mamlaka juu ya makamanda wa Polisi na hata majeshi mengine.

Wakubwa wa vyombo vya dola chini ya katiba na sheria hizi za wakoloni haziwezi kumpa nafasi kiongozi Mwadilifu yeyote ndani ya vyombo vya dola kama hataki kutumikia chama cha wenye madaraka. Hata kama ni mchapakazi na mwadilifu kiasi gani inabidi ajipendekeze na hata kuwanyanyasa binadama na ndugu zake waliopo upinzani ili kulinda madaraka yake yanayompa nafasi ya kutumbua mijihela kama wale waliohongwa mil 700 na kutaka kutorosha madini.
Hatujui michezo kama ile inafanyika kwa kiwango gani na nani hasa anairatibu. Wanaofanya hayo ni wazi kuwa wanajiamini kuwa ni sehemu ya kuwabeba Makada wa chama.
Kuna nchi moja kule America ya kusini mkuu mmoja wa vyombo vya ulinzi na usalama alikataa kushiriki wizi wa kura na kupindua matokeo kubeba chama Tawala ; alipohojiwa kwa nini anakataa kushiriki dhambi ya dhulma akajibu kwamba vyama vyote na wagombea wote ni wananchi wa nchi hiyo na wote walipewa nafasi sawa za kupiga kampeni kwa hiyo hawezi kumpendelea yeyote kwani itakua ni kinyume cha kiapo chake cha kutenda haki; kilichotokea ni watawala na chama chao kumtumia mkuu wa tume kufuta matokeo.
Baadae watawala wakashinda tena na wakamua kumsimamisha kazi yule mkubwa wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa madai kuwa ni mwanachama wa chama kikuu cha upinzani ,hivyo amekiuka katiba.
Alistaafishwa baada ya ushahidi kukosekana.

Chaajabu hakuna hata mbunge au kiongozi wa upinzani ndani ya nchi ile aliyewahi kumsemea popote yule muhanga wa kusimamia haki kwenye katikati ya mifumo ya dhulma ya kimadaraka.

Hili ndilo linalowafanya majeshi hasa wakubwa wao ambao wanapata maslahi mazuri na heshima kubwa kuamua kushirikiana na chama chenye kuwaweka kwenye fursa nzuri na kuwavurumisha mbali wapinzani wasioeleweka kuwa wamesimamia wapi juu ya kuendelea kubeba maslahi yao japo.

Tukirudi nchi za Afrika pia kuna tatizo sana kati ya vyama vya upinzani na vyombo vya dola.
Wapinzani wanacheza ngoma ya vyama tawala inayopigwa kwa kutumia majeshi kwa maana kuwa wapinzani wanatumia muda mwingi kulalamikia mfano Polisi bila kufanya utafiti na kujua shida zao na changamoto zao kisha kuja na Sera nzuri ya kuwakomboa, badala yake utasikia kuwa tukiingia madarakani tutalifuta jeshi la Polisi. Nani atakuruhusu uingie madarakani ili ukafute ajira yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom