Nafikiri cha muhimu ni kumuonesha mpenzi wako kuwa unampenda na kumjali. Mtu anaweza akawa na mapenzi ya kweli lakini anabaki nayo moyoni haoneshi kwa vitendo ili mwenza wake aone kuwa anampendwa. Kila mmoja anabaki na mapenzi yake moyoni, Matokeo yake kila mmoja anaishi kwa wasiwasi bila kuwa na uhakika kama aliye naye anampenda kwa dhati. Mazingira kama hayo yanaweza yakawa ni sababu tosha ya mmoja kutafuta mwingine ambaye yuko wazi akiamini kuwa huko ndio anapendwa.
USHAURI: Hakikisha mpenzi wako anajua kuwa unampenda si kwa maneno pekee pia kwa vitendo. Vitendo vinaweza isiwe ngono kuna mambo mengi ambayo unaweza ukamfanyia mpenzi wako na akajua kuwa unampenda.