Jicho la mwewe: ATCL saga

Zote kabisa!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mtoa hoja amekereka sana na riport ya CAG. Angetanani sana CAG abakie kimya ama aseme ni shirika lisilo na hasara wala faida yaani lipo kati aka uchumi wa kati.

Watanzania hatujazoea ustahamilivu wa kivisikia vitu tusivyovitaka!!
 
 
Wazee wakuchanganya gongo na bia ili tu kuidhinisha kwamba vyote ni vinywaji.
 
Apa nimekuelewa Bujibuji
 
Kuna pia wanaosema Serikali ingekodisha ndege badala ya kununua kwa fedha taslimu. Mbona hapo janga ndiyo lingekuwa kubwa zaidi kwa sababu tungekuwa tunalipa riba wakati tunaingiza kiduchu. Bora sasa hata kama tunaingiza kiduchu, lakini hakuna riba.
 
Sikujua kama kuna watu ni wajinga kiasi hiki, ila sikujua kabla kama bujibuji ni mmoja wao, unawezaje kufananisha huduma ya maji inayogusa kila mtu na ndege ambazo kama hazipo yapo mashirika binafsi yatafanya hiyo kazi na serikali kuepuka hasara? I think stupidity is your talent mr bujibuji or you attended stupidity class

Kubwa zima hovyoo
 
Naona mtoa hoja amekereka sana na riport ya CAG. Angetanani sana CAG abakie kimya ama aseme ni shirika lisilo na hasara wala faida yaani lipo kati aka uchumi wa kati.

Watanzania hatujazoea ustahamilivu wa kivisikia vitu tusivyovitaka!!
Hawa wakiwa mtaani ndo hulisha watu matango poli,
 
Watu hatuwazi Wala kulaumu ununuzi wa ndege, tunachohoji mbona tulikuwa tunaambiwa shirika limepata faida na kutoa gawiwo kwa serikali lakini kumbe linaendeshwa kwa hasara kubwa, je huko kurudisha ilikuwa n mradi wakutudanganya ili watuibie kwakisingizio hicho??

Hamna awamu iliyojaaa madudu na majizi kama ya Jpm.
 
Inawezekana kabisa kufupisha maongezi kwa hoja chache kama ifuatavyo.

MOSI, mwaka ule Nyerere alipokufa London, serkali ya Uingereza (nadhani ya Tony Blair) ilitoa offer ya kuleta mwili wake. Mkapa akakataa, akapeleka ndege yetu ya ATC na Rubani Ngandile.

PILI, mwaka karibu huo huo alikuja mgeni maaroof, raia wa Vatikano kule Italy, Papa Yohane Paulo II (sasa ni Mtakatifu Karoli Wojtyila). Alikuja kwa ndege ya Alitalia ingawa wakati huo SWISSAIR ndiyo ilikuwa inatamba.

TATU, Malkia wa Uingereza kila aendako hutumia British Airways (wao huita "flying the flag").

NNE, Wakati wa Vita vya Kagera, BOEING 737 ya ATC ilitumwa toka Mwanza hadi Dar es Salaam na Zanzibar kumchukua abiria mmoja tu, jina lake Muhidin Kimario wakati huo akiwa ni Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba. General Kimario alitoa mchango mkubwa tukashinda vita hiyo.

TANO, Tanzania, India, Brazil, Russia, Congo, ni nchi kubwa kubwa. Ema muwe na ndege zenu, au mlete Belgian Airlines za tundulissu. On the other hand, Israel , Switzerland, Qatar, Rwanda ni tunji tudogodogo, ndege kabla haijatulia angani imeshafika nchi jirani. Ona zinavyojaa ATC ya Dodoma, Mwanza, KIA, Mpanda, Iringa, au Songwe: je, huwa tunaokoa shilingi ngapi na tukileta ufanisi gani?

SITA, Maneno ya wapinzani hayana mantiki. Mtu amwulize huyu zittokabwe (alikuwa mwenyekiti wa PAC wakati huo) mwaka ule ATC ilipewa makaburu. What happened exactly? He will know, lakini for sure hakuna uzalendo pale.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba WHETHER ATC INAPATA FAIDA AU HASARA, VIGEZO VYAKE HAVIJAKAMILIKA. Kuleta mwili wa Nyerere ni gharama tupu, "expensive", haina kipato. Je, ni kweli haina kipato? Utaipa thamani gani safari hiyo? Abiria Kimario utamcharge shilingi ngapi?

Of course CAG ni Mhasibu, CPA Kadete, ana uzoefu mkubwa. Lakini audit yake imemfunga, inabidi atumie IFRS ambazo hazimjui Kimario wala Papa.

Uamuzi wa mwisho mie nashauri uende beyond IFRS.
 
Point ya watu ni ule uongo kwamba kulikuwa na faida. Ila ni kweli faida ya kuwa na shirika hai la ndege haiko kwenye balalance book pekee. Ni vizuri kufufua ATCL.
Tunasahau hapa kuna mambo mawili. Ndege ni mali ya Serikali pa se na ATCL wanakodi kufanyia kazi (lease). Sijawahi kusikia lessor amepata hasara tangu nipate akili. Hivyo aliyesema kapata faida ni lessor, mwenye ndege, hapa ndio serikali na waliogundulika kupata hasara ni ATCL mwendeshaji.
 
Kusomesha watu ni huduma kutibu watu ni huduma acha ufara
 
Kutetea haya ya ATCL kwa Ile 1-4 uliyoanza nayo pale juu utakuwa hujafikiria vizuri...nitazungumzia 1,3,4

1.Kwa vyovyote vile serikali ni lazima itoe mikopo ya elimu ya juu kwa kijana wa kitanzania

Hilo halitakuja kusimama kwa sababu ya hasara,serikali inakusanya kodi+vyanzo vyake vingine vya mapato ambavyo vina mhusu mtanzania na ndo maana kupitia hii wanajitahidi kufanya hata elimu ya msingi na sekondari kuwa bure...kwa hili hakuna hasara japo pesa za elimu ya juu inahesabika kama mikopo kana kwamba wafaidika wanatakiwa wailipe hapo baadae.

3.Kitambulisho cha taifa kinatolewa bure pia si hasara kwa serikali..ni muhimu kuwa na kitambulisho Kwa kila mtanzania na ndo maana serikali imebeba hizi gharama kwa kodi ya mtanzania mwenyewe...haijalishi pesa ngapi wanatumia lkn umuhimu wa hii kitu ndo maana zoezi likaenda for free of charge

4.treni ya abiria,umeme,maji na tiba hizi ni huduma za kijamii mzee. Haijalishi hasara ngapi wanapata hivi vitu lazma viwepo,na ndo maana kila mwaka wa bajeti hivi vitu vinapewa kipaumbele kwa sababu tutakuwa taifa la ajabu Duniani kama hakuna hizi huduma ila Dunia haitatuona wa ajabu kwa kutokuwa na shirika la ndege
.
.
Hayo hapo juu wala si biashara kwa serikali lkn hili la ATCL ni swala la kibiashara japo biashara ina faida na hasara sasa penye hasara lazma pajadiliwe na parekebishwe ili faida ipatikane...
 
Hii kitu umeeleza vizuri sana kwa sisi wataalam wa masuala ya air transport management tunakupa big up kwa kuielimisha Jamii ya kitanzania kwa wale wanaopenda kuelimishwa.
 
Nani alisema Lina faida, embu leteni evidence ya mtu alisema Lina faida, sababu mm binafsi sijawai sikia icho kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…