Kuna kitu watu pro-Muro mnaki-overlook sijui ni kwa makusudi, bahati mbaya au vyote. Muro pamoja na uzuri alionao kama binadamu wengine ana ubaya au udhaifu mkubwa wa kutochagua maneno ya kusema bila kujali nafasi yake na haiba ya timu anayoiwakilisha. Kama mshabiki, yuko vzr, ana hamasa, anazodoa, anaponda, anapambana na anajivunia timu yake.
Tatizo linakuja sasa pale anapokuwa amevaa usemaji wa timu bado anaendelea kuwa na notion ileile ya ushabiki. Kuna mambo ya kuzungumza on-air na off- air
Anazungmza bila kupima athari ya anachozungumza.
- Tulimsikia akilalamikiwa na Simba kwamba anatoa lugha za kashfa na matusi kwa Simba - mkamuunga mkono
- tukasikia akitoa lugha za kumdhalilisha Haji Manara as a person, mkaona sawa
- akamtukana kiongozi mmoja wa TFF kuwa yuko kama sanamu ya Michelin, mkaona sawa
- Akadhalilisha kabila la wazaramo, kwa kudai yeye ni mchagga, mkaona sawa tu
- Akamdhalilisha mwandishi wa habari mwanamke mmoja bila sababu za msingi, mkaona sawa tu
Amesema mengi tu mengine hata siyakumbuki, lakini kwa kuwa ninyi mashabiki wake hamkuweza kutofautisha tui na maziwa kama alivyokuwa akisema mwenyewe mara kwa mara, hamkuona kuwa kuna mahali anakosea na kumrekebisha, ninyi sasa ndio mliomponza. Na sasa badala ya kumsaidia atumie muda huu aliosimamishwa kujirudi na kujifunza zaidi mnaendelea kumpotosha ili akirudi asifanye kazi yake vizuri, badala yake mnataka akija afungiwe muda mrefu zaidi.