Wakati inaanza ilikuwa tamu ni kweli utamu wake zaidi ya asali, utamu wake ni zaidi ya sukari, mbinu na ubunifu zikatumika katika kuboresha "Jeclahay" nayo upendo na amani ukaongezeka naye watu wa karibu wakajuana.
Nayo furaha ikaongezeka nyuso zao zikavutia miili yao ikashamiri, lakini "shetani akaingilia kati" furaha ikayeyuka ikafuata tamaa, upendo na amani vikapotea hasira na visasi vikatawala, ndugu, jamaa, na marafiki wakakwaruzana hatimaye wakashikana mashati, mikwara ikapigwa hata moyo wa Iddi Amin ikajaa katika nafsi zao, nao wakatenda ukatili badala ya haki.
Yote haya inasababishwa na "Jeclahay" pesa imetumika, uongo umetumika, ahadi zimetumika, huruma ikatawala, nguvu nayo ikatumika, hakika watu wamepoteza maisha kisha "Jeclahay" vizazi vimepoteza watu muhimu kisha "jeclahay" laaaah..!
"JECLAHAY" ni nani?
Anawezaje kufanya yote haya mema na mabaya kwa wakati mmoja, JECLAHAY ni hodari aliye na visa vingi lakini mwisho wa safari yake kuna hatari.
Je ni nani huyu?
Jeclahay ni jina lenye asili ya kisomali maana yake ni "mapenzi"
Katika masuala ya mapenzi kuna njia ndefu lakini hakuna hata mmoja ajuaye mwisho wake, hivi karibuni tumesikia habari kuhusu kijana mwenye umri wa miaka 20 ameuawa kwa kusukumwa na mwenzake kutoka ghorofani katika hosteli ya chuo ya CBE, hakika ni majonzi na masikitiko, kisa ni mwanaume mwenzake kumuonea wivu na kuhisi anatoka kimapenzi na mpenzi wake lakini haikuwa hivyo, Leo hii kijana wetu David Shija kapoteza maisha tunakumbuka enzi zake alikuwa memba wa team cruiser hakika tumepoteza mtu muhimu.
Yote haya JECLAHAY ndiyo kasababisha, kuweni makini na huyu JECLAHAY muda wowote anaweza kufanya chochote "either" kwa ubaya "or" uzuri.
R.I.P
Shija.
May God be with you