Je, wewe ni mtu makini?

Binocular

New Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Habari wakuu.

Katika pitapita zangu za kimaisha nmejikuta nkipata experience nyingi sana kutokana na changamoto za kimaisha, nimejifunza mengi pia katika umri huu wa miaka 20's.

Wakati mwingine nimejikuta nkipata mawazo ya kufanya vitu vikubwa sana kama kijana nia na lengo ni kuzifikia ndoto kubwa za kimaisha nilizonazo.
Nimekuwa mtu wa kupenda kujifunza sana kila inapotokea fursa, hii imenifanya kukua sana kiakili, kuwa na confidence sana na kujitambua pia.

Mimi ni mwanafunzi wa chuo bado lakin nina experience kiasi kuhusu masuala ya kutafuta kazi, kufanya kazi na vitu vingine vingi!, nimewahi kufanya interview Tatu na zote nlifaulu vizuri, nimewahi kuajiliwa pia. Kiufupi nina uzoefu na vitu vingivingi na nmekuwa mtu wa kukubalika sana, hii ni kwa sababu kubwa ya kujitambua.

Lengo kuu la uzi huu ni kutaka kuzungumza na vijana wenzangu kuhusu uharisia wa maisha mtaani na pia nina nia ya kuanzisha platform ya vijana ila kupeana madini muhimu sana kuhusu movements za kimaisha.

Kiuchumi bado sijawa vizuri maana bado nina majukumu ya kimasomo hivyo imenipa ugumu kigodo katika kujihusisha na mishemishe zingine za kutafuta kipato, hii pia ni moja ya weakness niliyonayo kama binadam maana huwa ninapenda kujikita kwny jambo moja kwa wakati mpaka linapofikia mwisho(sipendi kuyumba).
Ukosefu wa mtaji pia unaweza kuwa sababu ya kutokuwa vizur kiuchumi kwa sasa, lakini nnachoamini mm tajiri maana nina ndoto na ideas pia.

Kwann vijana? hii ni kwasababu sisi ndiyo watendaji katika mishe zote za uzalishaji na utoaji huduma.
Tuna nguvu za kimwili na kiakili pia, hivyo tunapaswa kutambua umuhimu wa kuset mipango ya kimaisha katika kipind hiki ili itakapo fika umri wa kuitwa baba au mama tuwe tayar tushaiweka mipango katika utekelezaji.

KUHUSIANA NA PLATFORM HII.

Hii itahitaji watu makini sana (vijana) ambao watakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, pia tutahtaj kuwa na watu wakubwa (kiumri na namna nyngne) hawa tutawatumia kama washauri lakin shughuli zote za kiutendaji zitafanywa na vijana.

Nini lengo hasa?

● Kutengeneza kiwanda cha vijana makini kupindukia.
kutakuwa na trainings mbalimbali kutoka kwa watu wakubwa. Kutakuwa na fursa za kujifunza mambo mbalimbali yasiyopatikana shuleni.

● kutengeneza taswila mpya ya vijana.
Katika kizazi hiki wazee wamepoteza imani na vijana kwasababu vijana wamekosa awareness. Tunahtaji kurudisha imani zetu na tujengeneza kizazi chanya.

● kutatua matatizo.
Ni imani yangu kuwa kuna vijana wamejaaliwa uwezo mkubwa wa kudadavua mambo, tutahtaj kuwajengea vijana hawa uwezo wa kuface challenges, tutawatumia kutatua matatizo ya kijamii.

● litakuwa genge la kufua ideas zilizo tukuka.
Ninacho kiamin mm ni kuwa idea ndiyo chanzo cha kila unachokiona, tukianza kwa kuwekeza huku tunaweza fika mbali. Kutakuwa na kitu kama competition ya ideas kisha tutamove forward kwa kuziweka hzo idea kwny utendaji (hapa tutahtaji msaada wa taasisi husika)

Napenda kuchukua nafasi hii kukaribisha maoni na ushauri kutoka kwenu wakuu..

Nasubiria response ili niweze kuendelea na hatua inayofuata.

ASANTENI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…