Je, walemavu huhabarishwa?

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Posts
3,598
Reaction score
1,545
Habari wana JF,

Katika nchi yetu tuna wenzetu ambao ni walemavu(ngozi, macho, kusikia n.k).Katika kuhakikisha wanapata ufahamu wa yale yanayoendelea nchini na duniani/ulimwenguni, kuna haja ya kuwajali walemavu hawa mfano; wale wenye ulemavu wa kutosikia(Viziwi) wanapotazama vituo vya televisheni vya hapa kuwa na wakalimani/watafsiri wa lugha zao?
 
Mkuu hili nalo ni swala limekua likinisumbua kwa muda wikii hii nzima,
Nilikua najiuliza ni majengo mangapi yenye pavement za walemavu, au ni vyombo vingapi vya usafiri vyenye msaada kwa hawa ndugu zetu? Hata Ubungo Metro yetu iliyoanza safari majuzi ni taabu tupu kwa mtu wa kawaida kukwea ndani, najiuliza sembuse mlemavu?
Serikali na wakaguzi wa majengo wahahakikishe hawatoi vibali vya ujenzi kwa jengo lisilokua na miundombinu ya kuwasaidia walemavu.....!
 
Ni kweli Mkuu Mwanahisa, majengo yetu mengi hayazingatii njia za walemavu, inawezekana kabisa ajali nyingine nyingi tunazoziona kila leo ni kutokana na kushindwa kudhibiti hili!

Pili inapokuja katika suala la usafiri, hapa ndipo pengine penye utata, tunagombania nao(vipofu viziwi, katika barabara walemavu wa kusikia mfano(unaweza kuwa katika gari daladala au usafiri binafsi ukapiga goni sana tu lakini kumbe mtu ana matatizo ya kusikia)..

Once again, hawa watu wanapaswa kusaidiwa lakini tusipowafanya watambulika kwa kuwawekea misaada mbali mbali bado itakuwa ni shida!
 
MziziMkavu, Mbuzi Mzee...alama na viashirio vizuri sana hivyo(in JF photos)..vingekuwa vinawekwa katika mbao za matangazo katika taasisi mbalimbali..hata zikiwa barabarani na vituo vya kusubiri magari si mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…