Je Unamfahamu huyo Jamaa?

magabelab

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
374
Reaction score
202
Je Unamfahamu huyo Jamaa?

Yeye anajiita ChuraJasusi.

Wacha nielezee tabia za Huyu Jamaa.
TABIA
1.ChuraJasusi anapenda sana Microsoft os kama windows xp, windows 7 na 8.

2.ChuraJasusi anapenda sana kuajiriwa .Hivyo ukimweka kwenye mashine yenye windows , atatekeleza kitu chochote utakachomwambia kama
( a) Kutengeneza foda jipya
(b) Kufungua application yeyote iliyoko kwenye kompyuta
(c) Kunavigate file system ya computer mfano kwa wale wazee wa linux tumezoea kutumia "cd" ikiwa na maana na change directrory to. ChuraJasusi ukimwambia "nenda c:" ,Atakupeleka kwenye drive c. Hapendi kimombo kabisa huyu jamaa .
(d) kuangalia jina la mmiliki wa kompyuta
(e)kutengeneza file
(f) kufuta file
(g)kufuta foda
(h)kutengeneza path katika file system ya komputer
(i) kufungua na kuonyesha content za mafile aina ya .txt
(j) Kuangalia listi ya drives zilizopo kwenye computer
(k) Na mengine mengi coz anapokea command 29.
Angalia picha namba 1 upande wa kulia ili kuona baadhi ya command hizo.


3.ChuraJasusi anapokea Command kutoka computer yoyote hili yenye uwezo wa ku-telnet.
Picha 5 mpaka 8 inaonyesha nikitumia simu ya android kucontrol computer kwa kutuma maelekezo(command) kwenda kwa huyu jamaa ->ChuraJasusi

MAELEZO YA PICHA
Picha ya 1
Kushoto Inaonyesha nikidesign Picha ya huyu jamaa kwa kutumia software ya Gimp ,Picha hii nitaitumia kama icon.

Picha ya 2,3
Inaonyesha nikiprogramu (maelekezo) commands za huyu jamaa

Picha ya 4
Inaonyesha nikiwasha system ya huyu jamaa na kuweka namba ya port = 455 kwa ajiri ya telnet.
Namba ya port ni yoyote hile ambayo bado haijatumiwa na mashine .

Picha ya 5
nafungua telnet client kwenye simu yangu ya android. Telnet Inachukua ip address ya computer ninayotaka kui-control na port number ambayo tuliijaza kwenye picha ya 4

Picha ya 6
Nimefanikiwa kuunganishwa .

Picha ya 7
Sasa naanza kutuma command.
Nimetuma command ya "drv" ambayo ni sawa na kumwambia ChuraJasusi "tafuta drives zote kwenye hiyo computer kisha nitumia listi"

Picha ya 8
Kwa vile nimeshajua drive zilizopo.
Nimeweza kutuma command "nenda E:/"
ambayo imenipeleka drive E:\
kisha nikatuma command "lst" ambayo imemfanya ChuraJasusi aniletee listi ya mafile na foda zote zilizopo kwenye drive E:/ (E:\ ).
 

Attachments

  • 1.jpg
    169.7 KB · Views: 143
  • 2.jpg
    210.4 KB · Views: 119
  • 3.jpg
    116.7 KB · Views: 114
  • 4.jpg
    117.6 KB · Views: 112
  • 5.png
    7 KB · Views: 111
  • 6.png
    9 KB · Views: 114
  • 7.png
    9.8 KB · Views: 114
  • 8.png
    8.2 KB · Views: 125
Mmmmmm nahisi hii post ina wenyewe nimepotea njia samahani kwa kukatiza hapa kwa bahati mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…