taasisi nyingi za kutafuta maoni katu hazifanyi kazi bila kulipwa na yule anayezitaka. Sasa usambazaji wa matokeo si wa synnovate bali mlipaji. Kinachowasumbua synnovate ni kuwa matokeo yameonwa na wasiotakiwa kuona. Kama utafiti umelipiwa na ccm na matokeo hayawapendelei, basi ccm au yeyote atatumia ripoti hiyo kurekebisha mapungufu. Na mpinzani wa wake akiyapata atakandamiza kishenzi maana keshamkaba koo. Nakumbuka ngombale mwiru alipojibu kuhusu usawa katika vyombo vya habari vya taifa. Alisema " mnapogombana mieleka huwezi kumpa mpinzani wako kisu". Ripoti hiyo ni kisu kwa wapinzani wa ccm na wtakitumia ikibidi kumtegua kwenye mieleka hiyo!! Ukweli pengine, kwa wengine, ndio unaonekana sasa. He who pays the piper chooses the tune. Synovate is a business entity and will work for anyone who can pay them no matter what. They have to survive in this jungle.