doing your job is a revolutionary act.
Utashangaa mtu anapewa sifa kwa sababu tu "yule si mla rushwa".
Eboo, kutokula rushwa ndio tunavyotakiwa kuwa wote.Ukiwa huli rushwa ndo unafanya the bare minimum ya unayotakiwa kufanya, sasa hiyo inakuwa sifa kivipi? Kwa sababu watu wanaridhika na mediocrity?
Mzee Mwanakijiji alishawahi kusema kuwa Watanzania tunapenda sana drama! Tunakuwa kama tunasikiliza "Penzi Kitovu cha Uzembe" au "Aliyejuu". Tunasubiri wiki baada ya wiki kuangalia kuna nini kipya......
Wapo kweli kabisa ambao wamekaa kwenye viti vyao wanacheka kweli na kusifia kuwa "bunge letu kali sana" au "waziri huyo bomba sana" [kisa tuu kwa kutimiza wajibu wake] Really?
Tutafungukaje kama tunashangilia mazingaombwe na kupongeza viini macho? Tumeharibiwa na kitu gani kiasi kwamba tunaridhishwa na vitu vidogo kama watoto wanapopewa chuchu za plastiki kunyonya ili waache kulia!.....
Mojawapo ya falsafa za uongo (deceptive philosophy) zinazonezwa sana ili kuzuia watawala kuwajibishwa ni hii ya "kuona mazuri vile vile".
Kwamba, wananchi wanatakiwa waone mazuri ya kuyasifia ili watawala wajisikie vizuri. Ni falsafa ya uongo kwa sababu serikali kufanya mazuri siyo hisani na wala siyo 'optional'! Ni wajibu wa serikali kufanya mazuri na haiitaji kusifiwa kufanya mazuri.
Kwamba, serikali ikijenga barabara kwa kodi za wananchi isifiwe? Kwamba ikijenga hospitali hata kama hazina madaktari, nyenzo au madawa ya kutosha bado isifiwe kwa sababu ni jambo "zuri"?
Kwanini umsifie Waziri kwa kufichua ufisadi? Alikuwa na option ya kutofichua? Polisi akikamata mwizi asifiwe kwa kukamata mwizi? Alikuwa na option ya kutomkamata?
Watawala wanaotumia kodi ya wananchi kuleta maendeleo na watu hao waliomba kibali kuwaongoza wananchi hawana sababu ya kusubiri wananchi kuwasifia "kwa mazuri" wanayoyafanya? Jukumu la wananchi kuangalia mabaya yanayofanywa na kuimbia serikali kwamba haya ni mabaya! Kwa sababu si jukumu wala sababu ya serikali kufanya madudu!.....
Watu pekee wanaostahili sifa ni wale wanaofanya vitu kwa kujitolea na kujituma wenyewe si kwa sababu wanalipwa au wameajiriwa. Wakitaka kupongezwa vyama vyao viwaandalie sherehe ya kuzungumza vizuri bungeni na za kufichua ufisadi.
Kwa sisi wananchi hatutaki kuona ufisadi it is as simple as that. Kama hawawezi kufanya kazi au kutimiza wajibu wao bila kusifiwa waache!!!
Tunasifia mazingaombwe na kupongeza viinimacho