isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,152
- 6,601
| Jamhuri ya Peru / República del Perú / Republic of Peru
Peru ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka baina ya Colombia, Chile Bolivia, Brasil, Ecuador na bahari ya Pasifiki.
Taifa hili lenye ukubwa wa eneo zipatazo 1,285,220 Km[SUP]2 [/SUP]sawa na 496,226 Square Mile's ni nyumbani kwa watu takribani millioni 32,971,855 kufikia Juni 8, 2020.
Bendera ya Jamhuri ya Peru
Lugha rasmi ya taifa hili ni Kihispaniola pia lugha rasmi za upili ni Quchua na Aymara. Kauli kuu ya taifa ni "Uimara na Furaha kwa Umoja" | "Firme y Feliz por la Union".
Pesa rasmi ni Nuevo Sol (PEN), Sol 1 ni sawa na Centimos 100. Mji mkuu ni Lima, mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, kiuchumi na mji wenye maendeleo zaidi kwa taifa.
Jijini Lima, makao makuu ya Peru
Miji mingine yenye maendeleo ni Arequipa, Piura, Chiclayo, Tacna, Pucalpa, Iquitos, Chimbote, Ica, Huancayo, Cusco na Puerto Maldonado. Asilimia 90 ya miji yote hii imelalia upande wa magharibi katika uwanda wa milima ya Andes pembezoni katika fukwe za Pasifiki.
| Uchumi, Uwekezaji, Kilimo na Utalii
Taifa hili lenye ukuaji mzuri wa kiuchumi na sehemu salama ya kufanya uwekezaji, ni mshirika mkubwa wa mataifa ya Uchina, Marekani, Brasil, Chile, India, Japan na Uhispania.
Zabibu ya Peru ©PeruInfo
Uwekezaji ndani ya taifa unatokana na sera safi, matazamio na maazimio ya kina katika kupambana na umaskini. Kupitia viwanda vya samaki, vitambaa na mavazi, kemikali, vyakula, vinywaji na mbolea kumeifanya Peru kuwa taifa la 50 kiuchumi.
Peru yenye kutegemea uchimbaji wa mafuta, gesi na madini, uvuvi, utalii, kilimo, huduma za mawasiliano, kemikali na uchakataji wa bidhaa viwandani ni taifa la kipato cha kati.
Kahawa ya Peru ©PeruInfo
Kilimo ndani ya Peru huchagizwa na ardhi yenye rutuba kuwezesha kustawisha viazi, mahindi, mihogo, ngano, kahawa na matunda. Usafirishaji wa bidhaa tajwa kwa asilimia 40% kwenda nje ni moja ya kipato kwa taifa.
Parachichi za Peru ©PeruInfo
Utalii ndani ya Peru ni sehemu muhimu kutokana na historia za kale na uwepo wa pramidi za Machu Picchu. Sehemu muhimu zinazotembelewa zaidi na watalii ni jiji la Cusco, Milima ya Huascaran na Coropuna.
Machu Picchu ©Hastaya Maya
| Elimu, Sayansi na Afya
Kiwango cha elimu kwa taifa ni asilimia 94.17 kufikia Machi 25, 2020 kwa mujibu wa Instituto Nacíonal de Estadística e Informatica (INEI). Elimu ndani ya Peru ni bila malipo (Bure!) na lazima kwa elimu ya awali, msingi na upili, huku elimu ya juu ikitolewa fedha za kujikimu. Baadhi ya vyuo bora ni National University of San Marcos, Universidad Peruana Cayetano Heredia, Universidad de Piura, Universidad Tecnológica del Perú na César Vallejo.
Peru katika sayansi ya anga za mbali inawakilishwa vyema na mwanasayansi Carlos Noriega anayefanya shughuli zake chini ya mwavuli wa NASA, SpaceX na ESA
Huduma za afya hutolewa bila malipo katika hospitali za umma, hospitali za umma vitengo maalumu vya meno, watoto, mifupa na uzazi na hospitali za jeshi la wananchi wa Peru.
| Michezo, Sanaa na Filamu
Mchezo pendwa ni mpira wa miguu, Peru inawakilishwa vyema na timu ya taifa katika mashindano ya kimataifa ikiwa nyumbani kwa wachezaji nguli Claudio Pizarro mwamba aliyecheza mpira na mpira ukamcheza, akivitumikia vilabu vya FC Bayern München, Werder Bremen, FC Köln na Chelsea.
Claudio Pizarro ©Werder Bremen
Wachezaji wengine waliopeperusha bendera ya Peru ni kiungo matata wakati huo Norberto Solano, Paolo Guerrero, Sergio Peña na Jefferson Farfán.
Peru ni nyumbani kwa mwandishi, mchoraji na mwanafalsafa Carlos Enrique Dolanco mwenye heshima yake ndani na nje ya mipaka ya taifa.
Claudia Llosa ©Berlin Post
Filamu ndani ya Peru imewakilishwa vyema na mwanamama Claudia Llosa muongozaji, mwandishi na mzalishaji wa filamu ya 'La teta asustada' | 'The milk of Sorrow' Filamu hii iliyoandaliwa kwa ushirika na Marco Castro na Fransisco Lombardi ilifanya vyema ulimwenguni kote.
Peru ni taifa la kwanza Amerika ya Latini kuzalisha filamu ya kwanza ya 3D inayofahamika kama Piratas en el Callao. Filamu nyingine zilizochakatwa ndani ya Peru ni Eternity na The Bad Intentions.
Hii ndio Jamhuri ya Peru 🇵🇪