TAARIFA KWA UMMA
Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na mtandao wa
matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo
Wapka.mobi.
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayo
inamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia
sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyote
mwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulipa ada ya shilingi 37,000/=.
BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE
NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa
ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013 ...........matAPELI HAO