Its now official: Vodacom na Tigo wapambana kuinunua kampuni ya Zantel

mdhalendo

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
282
273
Baada ya kampuni ya simu ya Zantel kuendelea kupata hasara mfululizo, kampuni ya Etisalat inayomiliki asilimia 65 ya hisa za zantel imeamua kuuza hizo ili kujiondoa kwenye soko la simu hapa nchini.

Zantel ambayo licha ya kupanua wigo wa mtandao wao tanzania bara lakini imekosa mvuto kwa wateja wa tanzania bara. Kampuni kubwa za vodacom na tigo zinashindana ili ziweze kumiliki mtandao huo wa Zantel.

Hali kama hiyo iliikuta kampuni ya Yu Kenya ambayo pia illiingia hasara mfululizo mpaka iliponunuliwa na Safaricom na Airtel Kenya.Baada ya kampuni ya simu ya Zantel kuendelea kupata hasara mfululizo, kampuni ya Etisalat inayomiliki asilimia 65 ya hisa za zantel imeamua kuuza hizo ili kujiondoa kwenye soko la simu hapa nchini.

 
Kama wateja wa Zantel wangekuwa na uamuzi wa nani anunue Zantel, nadhani wasingekubali kununuliwa na Voda wala Tigo maana ni balaa. Kwa hiyo wateja wa Zantel zile huduma mlizokuwa mkizipata kwa kujinafasi ndio mwisho. Poleni!!!!
 
Kama wateja wa Zantel wangekuwa na uamuzi wa nani anunue Zantel, nadhani wasingekubali kununuliwa na Voda wala Tigo maana ni balaa. Kwa hiyo wateja wa Zantel zile huduma mlizokuwa mkizipata kwa kujinafasi ndio mwisho. Poleni!!!!
bora kabisa zantel ipotelee mbali.
 
hawataki zantel ila wanataka mkongo wa baharini unaomilikwa na zantel,kama nchi ilitakiwa iwahi inunue iwe ni mali ya taifa,sio makampuni binafsi,

Zantel hawamiliki mkongo baharini mkongo unamilikiwa na seacom..zantel wana miliki gateway ambapo voda na tigo hawana
 
Kampuni mpya za mawasiliano ambazo hazijipangi kisawasawa zitaishiaaaaa kufirisika na kuuuzwa tu...

Sasatel walikuja kwa mbwembwe.........kudadekiiiii chaliiiiii

Zantel ndo kifo cha mende.

Smile , vietel mjiandaeeee.
 
hawataki zantel ila wanataka mkongo wa baharini unaomilikwa na zantel,kama nchi ilitakiwa iwahi inunue iwe ni mali ya taifa,sio makampuni binafsi,
Hao watunga sera ndio wamiliki wa vodacom so hawawezi kuacha serikali imiliki zantel maana wao watakosa faida.
 
soko la makampuni ya simu limeshakuwa saturated kwa hiyo kwa kampuni mpya kupenya na kunyanganya wateja wa kampuni ambazo zipo ni ngumu sana!
 
hv zantel sio voda? mbona wanatumia.....moja?/tafitini! wazalendo! hawa ni kaka na dada ispokuwa dada alihamia znz kijanja!
 
ingekuwa vizuri hii kampuni ingebadirisha mfumo wa biaahara kutoka mfumo wa simu na kwenda ktk mfumo wa kugawa internet connection tu. hapa ndio napojiuliza Tanzania haina matajiri wa kununua na kuendesha kampuni km hizi, shoprite imeuzwa tunaiyona kisa matajiri wetu hawawezi kuweka nyanya za Iringa na mayai ya Kitunda.
 
Zantel own Eassy Submarine Cable!!!

IPO HIVI WADAU, KWANZA SEACOM NA EASSy NI WASHINDANI KATIKA BIASHARA, NA WOTE WANATUMIA FIBRE CABLE SARE ZA NJIA MBILI (640Gbs X 2) KWA SEACOM NA (700Gbs X 2) KWA EASSy NA KILA MMOJA AKIWA NA CABLE ZAKE, EASSy AKITOA MTUNZINI AFRIKA YA KUSINI NA SEACOM AKIUNGANISHWA KUTOKEA MUMBAI INDIA, ZANTEL NI PARTICIPATING PARTERS(WAKO 13) WA KAMPUNI YA INDIA, WEST INDIAN OCEAN CABLE COMPANY (WIOCC) NA TTCL AKIWA NI PARTNER WA MOJA KWA MOJA WA EASSy, HII NI KUSEMA ZANTEL WANARIPOTI WIOCC NA TTCL WANARIPOTI EASSy, ILA YANAYOFANANA HAPA NI KWAMBA SEHEMU YA MKONGO KUTUA NI MMOJA NA SEHEMU YA KITUO CHA KUENDELEZA(ONWARD CONNECTIVITY) NI KIMOJA KIPO KIJITONYAMA, INGAWA KWA MIKATABA TOFAUTI, NA KWA KUMALIZIA SEACOM UMILIKI WAKE WOTE NI WA BINAFSI WAKATI EAASy UMILIKI WAKE NI MUUNGANIKO WA MAKAMPUNI YA MAWASILIANO 20,NA WANAPATA FEDHA KUTOKA IFC(KITENGO NDANI YA WORLD BANK) NA MASHIRIKA MENGINE YA KIFEDHA KWA AJILI YA MAENDELEO
 
Biashara ushindani ni mkubwa mno Zantel inafanya vema Zenji wajizatiti zaidi huko kwakuwa hata hivyo ndio chimbuko lao

Nitawakumbuka kwa mengi na mojawapo ni kutuma pesa kwa kutumia simu, Zantel ndio wa kwanza kuleta hiyo huduma nakumbuka kama sikosei ilikuwa way back 2007, ilikuwa kitu cha ajabu kweli nilimtumia mtu pesa Mwanza na akapata, leo wamepigwa jumbo ni mwendo wa tigo na mpesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…