PreGE2025 Issa Gavu: Marufuku uonevu, chuki, fitina na uzushi kwa lengo la kuwawekea vikwazo wanaotaka kugombea CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Issa Ussi Gavu, Katibu wa NEC ya CCM anayeshughulikia Oganaizesheni, amesisitiza kuwa ni marufuku kwa wanachama wa chama hicho kufanya vitendo visivyofaa kama vile chuki, uonevu au kuzushiana tuhuma kwa lengo la kuwazuia wengine kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Temeke, Gavu alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa wagombea wake wanapatikana kwa haki na kwa njia halali, na kwamba hakitakubali michezo ya hila katika mchakato huo. Alifafanua kuwa ushindi wa chama katika uchaguzi utatokana na wagombea wanaokubalika kwa wanachama, wenye sifa stahiki na waliochaguliwa kwa uwazi.

Alisema kuwa hakuna mwanachama mwenye nia ya kugombea ubunge au udiwani atakayekatwa kwa chuki au hujuma. Vikao vya uteuzi kwenye ngazi ya wilaya na mkoa vimetakiwa kusikiliza wagombea, kuwapa nafasi ya kujieleza, na endapo kuna kasoro, basi hatua zichukuliwe kwa haki.

Gavu alionya dhidi ya tabia za "kukata kihuni" ambapo baadhi ya watu huwekewa tuhuma zisizojulikana na kunyimwa nafasi ya kujitetea. Alisisitiza kuwa kila mwanachama ana haki ya kugombea, na mchakato wote lazima uwe huru, wazi na wa haki.

Aidha, alieleza kuwa CCM inalenga kupata viongozi waadilifu, wenye uwezo wa kuwawakilisha wananchi kwa weledi. Alisema chama kina wanachama zaidi ya milioni 12, na kati yao ni lazima wapate viongozi bora bila kuvuruga utaratibu wa ndani.

Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa nafasi za uongozi ndani ya chama si za kununua au kutengewa kwa misingi ya fedha, bali ni kwa wanaCCM waliotumika, waliolelewa na walioandaliwa kutumikia wananchi kupitia chama.
 
Hapa kuna lengo la kuwapa nafasi walioandaliwa kwenye Uislamu .
 
sasa haya MACCM yenyewe kwa yenyewe yanafanyiana figisu!unategemea nn kwa wapinzani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…