Habari za muda huu.
Bila kupoteza muda,naelekea moja kwa moja kwenye mada tajwa.
Kwa wale ambao tunapenda kuifuatilia dunia yetu,hasa kwa upande wa masuala ya anga,ni wakati muafak wa kupakua Application hii inayopatikana Google Play kwa wale tunaotumia simu za Android.
App hii imetengenezwa na shirika la marekani linalosimamia masuala ya uchunguzi wa anga,hususani anga za mbali lijulikanalo kama NASA(National Aeronautics and Space Administration).App hii inakupa nafasi ya kuona majira mbalimbali kwa wakati muafaka katika dunia ukiwemo usiku na mchana.Pia inakuwezesha kuona mahali jua au mwezi vilipo kwa wakati husika.Chombo hiki huizunguka dunia kwa kasi sana,kama utakavyoona hapa chini kwenye picha.
Binafsi,napenda sana kuichunguza dunia,lakini,bahati ya kusomea kiundani masuala haya iliniponyoka baada ya kupata alama hafifu kunako NECTA miaka hiyo,licha ya hayo yote moyo wangu husuuzika sana ninapoitumia App hii,kwani huwa najihisi na mimi ni mwanasayansi kamili.Picha ya mwisho kabisa inaonesha muda kifaa hicho kilipokuwa kipindi nachukua screenshot hiyo.
Na kifaa hiki kinaizunguka dunia kutoka Magharibi kwenda Mashariki.
Jaribuni kuipakua mjionee mambo makubwa,siyo kukesha Instagram na WhatsApp tu.
Simu yangu ni ndogo lakini naitendea haki.Kazi kwenu.