Ishi Kama penseli ili uwe mtu bora

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,401
Reaction score
7,900
Mtengenezaji wa penseli alipomaliza kuitengeneza penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.

“Kuna vitu sita unatakiwa uvitambue, kabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.”
Alisema mtengeneza penseli.

MOJA----Utakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wako”

“MBILI" utapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.”

TATU--- utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya..

NNE---kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika. Hivyo kilinde

TANO---Alisisitiza mtengenezaji penseli, “kwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki tuu.

“NA SITA-- Ipo siku utaisha na kupotea kabisa. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu niliokwambia kuufanya..

PENSELI ilielewa na kuahidi kuyakumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.

Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.

MOJA---, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa katika Maisha yako, ikiwa utajiweka kwenye mikono ya MUNGU.

MBILI---, utakutana na magumu mengi na yenye kukuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, hivyo usiyakimbie.

TATU---, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya nyuma. Usijilaumu kwa uliyoyafanya nyuma.

NNE---, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyoko ndani yako kwani ndiyo inayoandika hatima ya maisha yako. Hivyo Ilinde.

TANO---, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa Viwango vya juu.

SITA--, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani, na utaonekana Kama mzururaji tuu.

Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumbaji wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza kusudi ulilotumwa na Muumbaji WAKO.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nalo ni neno jema Mkuu linafaa kwa maarifa
 
🤣 🤣 🤣 do! penseli fupi lakini itaisha haraka
 
msg nzuri kwa kweli
 
Penseli Penseli Penseli 😍
 
Hizi story ni nzuri,ila kwa Afrika tu,
Inabidi twende mbali zaidi watu kama Bill gate,Eron musk,Dangote,Jeff bezoz,walipokuwa wadogo walifundishwa haya?au wao wanawalea vipi watoto wao?
Maana huku Afrika hata mtoto wa Raisi Richa ya kupewa Elimu nzuri na fulsa lakini wengi hawana uwezo wa kuanzisha kitu chao kama kampuni,zaidi watabebwa na kupachikwa kwenye ajira nono tu,lakini hawana maajabu kabisa !!
Ni tofauti na mtu mweupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…