Aisee hii ni very good debate:
Jana nilipoangalia ile hotuba ya Khamenei nimepata wazo kwamba ile system ya Iran inawafaa:
1. ile ni system ambayo ni blend kati ya religious sytem na secular system. Upande mmoja unatoa spiritual guidance na upande wa pili unatoa secular guidance, ili Iran iwe stable inahitajika hizi system zifanye kazi vizuri, busara, hekima inabidi vitawale sana lasivyo kutakuwa na mikwaruzano isiyoisha.
2.Iran kama taifa liliokuwa chini ya Ufalme kwa miaka mingi(rejea persia empire) na pia ufalme wa juzi hapa ule wa Shah uliong'olewa, ni taifa ambalo uwepo wa strong man umekuwa ni sehemu ya culture yao,kwa zamani role hii ilikuwa ikishikwa na mfalme lakini kwa sasa imeshikwa na Ayatollah, japo at the same time kuna modernization ambapo raisi anachaguliwa kidemokrasia.
3.Iran ikifuata Western System nadhani haiwezi kuwa stable, kwa sababu system ya west haiblend na culture yao ambayo ni partly ufalme ufalme plus spirituality plus modernization, Western system itaondoa umoja wa wairan na kusababisha civil tensions.
4. kwa jinsi kwamba serikali ya Bush iliwahi kukiri kwamba kuna budget maalum ya kuidistabilize Iran, siwezi kuona ni kwa namna gani Marekani haijatia mkono katika suala hili.
5. Irani kuviblock vyombo vya habari kama BBC mimi ninaona sawa, hasa ukizingatia role iliyoplay BBC Persia Channel katika kuuangusha utawala wa Waziri mkuu Mossadegh, pale ambapo BBC persian channel ilipokuwa ikituma Coded messages ambazo wapinduaji walikuwa wakitumia kuwasiliana.
6. Iran itaibuka katika mgogoro huu ikiwa very much Stronger, kwa maana haki itakuwa ni jambo ambalo Viongozi wa Iran watakuwa macho nalo.
7. Mousavi nguvu yake ni power of the moment, yeye binafsi nadhani atakuwa anahofia fate yake na legacy yake ndo maana anajaribu kuwatumia waandamanaji ili apate better deal haraka iwezekanavyo, na at the same time waandamanji siyo kwamba wanamzimika Mousavi kihivyo, bali nao wanamtumia ili waweze kupeleka ajenda yao mbele.