Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo imefanya majaribio ya makombora ya masafa marefu yaitwayo Shahab-3 na mengine yaitwayo Sajjil, ambayo yana uwezo wa kusafiri hadi kilometa 2,000 (maili 1,240 ).
Jeshi maalum la Iran liitwalo The Revolutionary Guards limefanya majaribio hayo ambayo ni sehemu ya mazoezi ya kivita yaitwayo "Sacred Defence Week".
Makombora hayo yana uwezo wa kufika katika nchi ya Israel na sehemu yote ya ghuba ya uajemi ambako kuna vituo na vikosi vya kijeshi vya Marekani katika nchi ya Qatar. Pia nchi za Bahrain, UAE, Saudi Arabia na Kuwait, sehemu za Ulaya hasa Uturuki, zinakuwapo kwenye mlengo.
Kitendo hiki cha Iran kujaribu silaha hizi kinashabihiana na kitendo kilichofanywa na Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini mwezi June mwaka huu ambapo nao walijaribu makombora ya masafa marefu na kusababisha kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa.
Baadae Pyongyang wakasema kwamba wamefikia hatua ya mwisho ya kurutubisha kemikali ya Uranium na walikuwa wakikoleza makali ya plutonium.
Korea ya Kaskanzini inaaminika kuwa na plutonimu ya kutosha ambayo ni mabomu sita ya atom.
Wiki ijayo waziri mkuu wa China Wen Jiabao atakwenda North Korea kukumbusha kuwepo kwa mazungumzo ya kuhusu mabomu ya nyuklia ambapo nchi sita ikiwemo US, Russia, South Korea na Japan zitashiriki.
Mwanzoni mwa mwaka huu North Korea ilijitoa katika mazungumzo hayo baada ya kulaumiwa kwa kitendo chake cha kujaribu makombora ya masafa marefu.
Alhamisi ijayo Iran itafanya mazungumzo na nchi wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la UN liitwalo 5+1 US, France, Britain, Russia, China na Germany kuhusu malengo ya silaha zake hizi.
Yaani ni hekaheka tupu!