Iran itatoa jibu kali

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Brigedia Jenerali Baqeri: Hatua yoyote dhidi ya Iran itajibiwa vikali zaidi

Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amezungumzia harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kueleza kuwa Marekani itakabiliwa na jibu kali iwapo itachua hatua au kutaka kuteteresha usalama wa Iran.

Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu na majeshi yake yote vinasimamia kwa makini maeneo yote ya mipaka ya nchi kavu, anga na baharini na kufuatilia kikamilifu harakati zote.

Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa harakati za kijeshi za Marekani huko Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi zinapigiwa debe na makelele mengi katika vyombo vya habari vya vibaraka wa Marekani dhidi ya wanamuqawama huko Iraq na kikosi cha wapiganaji wa kujitolea cha wananchi cha al Hashd al Shaabi.

Brigedia Baqeri Baqeri amesisitiza kuwa viongozi wa Marekani wanafahamu vyema kwamba wananchi wa eneo hili wakiwemo wa Iraq wanapinga kuweko majeshi ya nchi hiyo katika nchi hizo.

Harakati za kijeshi zinazotia shaka za Marekani za kuwahamisha wanajeshi wake huko Iraq sambamba na ripoti zinazosema kuwa Washington inafanya mipango ya kuyashambulia baadhi ya makundi ya muqawama wa Kiislamu na lile la al Hashd al Shaabi, vimeibua wasiwasi ncini Iraq.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona bado hatutoshi km Dunia mpaka wengine wanahangaika na matakataka ya vita?
 
Marekani ni dhaifu Sana leo kuanza kuwaza kuwashambulia Iran.. wanamaji wao wsnakosa morali Lisa korona,
Wairan vile vile.. lakini si Salama kabisa kumjaribu Iran au marekani katika kipindi hiki coz kila mmoja atataka kuonyesha utayari wa Vita hata katika kipindi kigumu Kama hiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…