Ipi asili ya ujangili ?

Joined
Feb 14, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Wakati wengi wakitafakari na kupambanua nini kifanyike ili kutokomeza na kufutilia mbali biashara haramu ya ujangili unaotishia kutoweka kwa wanyama katika dunia.
Wakati wengine wakitafakari kupambana na ujangili,majangili watakuwa wanatafakari mbinu nyingine ya kupambana na wapinga ujangili.
Hii inatokana uhalisia wa wengi kuunda mbinu pale wanapogundua kuwa kuna watu wa upande wa pili wakiwapinga.
Wakati dunia ikitafakari na kupambanua nini kifanyike ili kutokomeza ujangili,wengine wanamwaga machozi na maumivu ya madhara ya ujangili lakini leo sitozungumzia maumivu hayo.
Wakati tukitafakari kutokomeza ujangili,tunapaswa pia kutafakari NINI ASILI YA UJANGILI ili kusaidi ujangili huo kutoweka na kupotea kabisa.
NINI ASILI YA UJANGILI ?
NANI ANAFANYA UJANGILI ?
WAPI MAJANGILI WANAPOPELEKA NYARA ZAO ?
VIPI MAJANGILI HAO WANAFAIDIKA NA TAIFA LINAPATA HASARA
ni maswali machache sana lakini yenye uwezo wa kuleta suluhisho kwa asilimia fulani.
Pindi tutakapo jua kuwa ASILI YA UJANGILI ni biashara haramu inayolitia taifa ktk hasara kubwa ndio siku ambayo wengi watapata machungu na kuwa wazalendo na taifa lao.
ASILI YA UJANGILI NI NINI ?,nani aliwahi kujiuliza swali hili ?
Hilo nalo ni jambo jingine la muhimu,na inawezekana wengi wameshajiuliza swali hilo lakini majibu yao yamekuwa magumu kupatikana.
Katika kuijua asili ya ujangili itasaidia kumjua jangili mwenyewe.
Kwani hakuna mtu anaeweza kufanya biashara isiyo na faida na kwenye biashara yoyote lazima kuwe na muuzaji na mnunuzi.
Mnunuzi anapokosekana basi muuzaji na yeye hatokuwepo.
Kwani biashara ni faida.
ASILI YA UJANGILI ni kuwafahamu pia na wale ambao wananunua malighafi hizo.
Kwani tunapaswa kupambana na wengi na siyo wachache.
Kuijua ASILI YA UJANGILI NI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI.
Kwa maoni na ushauri: ningawildlifefoundation@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…