iPhone 6 plus

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,980
Reaction score
4,284
Wadau,

nina tatizo, jana ''nili-restore to factory settings'' iPhone 6 plus, nilimaliza wakati nafanya set up ikahitaji password ya account ya iCloud, kwa kweli mwenye simu hakumbuki password na mpaka sasa sijui tufanyaje.
Tumepitia mitandao mbalimbali ikiwemo apple.com na kwa kweli njia pekee ya kufanya hii simu kutumika tena ni kukumbuka password ya iCloud maana ilisetiwa kwa ajili ya security iwapo ingepotea ''find my iphone''.
Wadau kuna namna nyingine ya kufanya maana nimejaribu kutumia apps za ku-bypass icloud account lakini sipati functions zote za simu.

Msaada na ushauri wako ni wa maana sana.
 
nenda posta jengo la mavuno house ulizia fundi anaitwa baker ila ni gharama sana kama laki tano
 
Mwny nayo kasahau password?rudisheni Simu ya watu nyie,huweZi fanya chochote kama huijui hy password ya iCloud
 
Labda mwenye nayo kasahau na email password yake....😁😁 Mi situmii apple na si fan wake sana ila hapa nawakaubali. Kama simu si yako hufanyi chochote
 
Mkuu hakuna mtu anaweza kuitoa hiyo lock utahangaika sana

Btw nimepoteza iphone 6+ isije ikawa ndio hiyo umeuziwa mkuu

If so check na mimi pm tumalizane
 
Haiwezekani mwenye simu asahau password zote yaani ya iCloud na password ya email yake unless ni simu ya wizi hiyo
 
nenda posta jengo la mavuno house ulizia fundi anaitwa baker ila ni gharama sana kama laki tano

Mkuu usimdanganye mwenzio kumbuka hiyo ni iCloud password na sio pattern password au network lock
 
Acha uongo iphone unaporeset lazima uweke password ya icloud umereset kwa itune au hii ni ya kupigwa mtafuteni mwenye cm mmpe cm yake ilo ni kopo kwenu
 
Mwny nayo kasahau password?rudisheni Simu ya watu nyie,huweZi fanya chochote kama huijui hy password ya iCloud

Problem solved at last mke wangu amekumbuka password yake.
Next time tumia akili kufikiri, kwa kuwa wewe ni kibaka unahisi kila mtu ni kibaka?
 
Acha uongo iphone unaporeset lazima uweke password ya icloud umereset kwa itune au hii ni ya kupigwa mtafuteni mwenye cm mmpe cm yake ilo ni kopo kwenu

Acha kukurupuka, ukiwa kwenye mitandao usihisi kila mtu ni kama wewe......

Na katafute basi uibe ili uwe na kopo la iphone

Problem solved at last mke wangu amekumbuka password yake.
Next time tumia akili kufikiri, kwa kuwa wewe ni kibaka unahisi kila mtu ni kibaka?
 
Wadau,

Wife amekumbuka password yake baada ya kulia kwa masaa kadhaa na sasa simu yake ipo poa kabisa, shukrani kwa wale walichangia kwa kutumia akili;
Kwa wale waliokurupuka kwa hisia, nawapa rai wanapokuwa kwenye mitandao ya kijamii wapunguze mihemuko maana wengi walikmbilia kwenye wizi.
Shukrani.
 
Mkuu hakuna mtu anaweza kuitoa hiyo lock utahangaika sana

Btw nimepoteza iphone 6+ isije ikawa ndio hiyo umeuziwa mkuu

If so check na mimi pm tumalizane

Mkuu,
Huwa situmii vya wizi, hii niliinunua wakati huo safari za nje zilikuwa hazijasitishwa, so pole kwa kupoteza simu yako.
Na bahati nzuri wife amekumbuka password yake, so tatizo limeeisha.
 
hata kama umesahau pwrd si ariset tu aende kwenye email yake aingize hiyo paswrd mpya

Thanks ulitoa ushauri mzuri na unaofanya kazi...
Bahati nzuri wife katika kujaribu alikumbuka password yake.
Cha muhimu ni kuwa na taarifa za icloud account.
 
mwanzo ulimtambulisha kama mwenye simu...endelea tu kumtambulisha kama mwenye simu achana na wife!
 
akuna cha amekumbuka password wala nini umeona hakuna msaada unazuga umeshamaliza tatizo pumzika kwa amani acha niendelee kukurupuka na wengine waliosahau apple Id zao ilo no kopo uza spear mfundi watoe kioo na battery watuuzi wateja ambao hatujasahau apple id zetu vikaba ambao tunakumbuka apple Id zetu wenye mali mnaosahau Apple Id acha ukanjanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…