Innocent Killer (The Revenge)

JIJI LA KAMALI ( GAMBLING CITY)

INTRO...........
Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini.

Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika.

Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu sana na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini sana kwa hapo ambapo alikuwa amesimama.

Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia sana mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini sana kwenye jambo hilo hivyo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo.

Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sana sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mno mithili ya radi ya mvua.

Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka sana ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka.

Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safari kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali na kumfanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu.

Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu sana.

Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa.

Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mno mpaka umeme ulipo katika ghafla sana ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini sana maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya sana na umeme huo kukatika alishukuru sana japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa.

Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla sana na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu sana ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua.

Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya sana begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa.

“KAMALI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMALI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo. Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe sana.

Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMALI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda?

Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMALI.

Simulizi hii inasomwa kwenye group la WhatsApp tu pekee na haitapostiwa mahali pengine popote hivyo nicheki haraka nikuunge kwenye group langu la WhatsApp uanze kusoma simulizi hatari sana ya watu wenye jiji lao la KAMALI (ni hatari sana).

Kujiunga bei yake ni shilingi 3000 tu, yaani ukilipia 3000 nakuunga kwenye group haraka sana.

Usikae kinyonge wakati naingia kujifungia ili ufurahi na kwenda kuisherehekea vyema likizo yako ndefu. Maandishi yapo yanakusubiri wewe tu, usijibane ukataka kukosa simulizi hii bora ya kusisimua eti kisa 3000 tu.

Lipia kupitia namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote FEBIANI BABUYA

Nataka watu 30 tu wa mwanzo nianze nao haraka sana, unaweza kuwahi kabla nafasi hazijajaa ili usije ukaikosa


Niwatakieni asubuhi njema.

Kalamu ni yangu mwenyewe;

FEBIANI BABUYA.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tumebakiwa na episodes 38 ili kumalizana na simulizi hii mpaka mwisho sehemu ya 135.

Natoa ofa kubwa. Malizia hizo episodes zote kwa shilingi 1000 tu.

1000 yako inakufanya umalizane na hii simulizi leo leo.

Lipia kwa namba

0621567672 (WhatsApp)

0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Wasalaam.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)-Simulizi mpya na bora sana ya kipelelezi/kijasusi imetoka rasmi kwa mfumo wa softcopy (nakala laini)

Hii ni moja kati ya movie bora sana iliyopo kwenye maandishi ambayo utaisoma mwaka huu....Kuna mwanaume alipigwa zaidi ya risasi sita kwenye mwili wake kisha akaenda kuzikwa akiwa hai.......Alizikwa porini ambako hakukuwa na binadamu yeyote yule anayeishi LAKINI cha kushangaza mwanaume huyo alikutwa anaishi na yupo hai miaka kumi na mbili iliyo fuatia baadae.....Walichanganyikiwa na ndipo alitumwa BEAST mmoja kwenda kumtafuta ili kujua mtu aliyezikwa anakutwa vipi mtaani! Ni bonge moja la simulizi
NICHEKI UJIPATIE NAKALA YAKO LAINI uendelee kufurahi.....


Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 5000 tu.

Nicheki WhatsApp kwa namba 0621567672 uweze kuipata yako.

Kama unalipia namba za malipo ni hizi hapa


0621567672

0745982347

FEBIANI BABUYA.

Karibu tuyafurahie maandishi, ndipo chanzo kikubwa cha akili na maarifa kilipo jificha
.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Imalizie kwanza hii boss
 
Huyu jamaa sijui vipi. Mahadithi kibao hayana hata mwisho.
Ni hadithi ngapi ambazo hazina mwisho?


Nimeleta ULIMWENGU WA WATU WABAYA...nilimaliza mpaka mwisho.

Nikaleta I WANT TO DIE JUDGE.....Nikamaliza mpaka mwisho.

Nikaleta GEREZA LA HAZWA.....Nilimaliza mpaka mwisho.


INNOCENT KILLER pekee ndo niliishia 100...
Sikumaliza kwa sababu zangu maalumu.


Now DOCUMENT NUMBER 72 inaendelea.


Kwa hayo maelezo yako ya mahadithi kibao hayana hata mwisho unajiona upo sahihi?


Kuna muda wasapotini waandishi hata kama sio mimi, wengine wasapoti tu. Waandishi wengi wanaandikia kwenye mazingira magumu sana na kuna watu wanatumia muda wao mwingi sana kwenye uandishi.

Kuna watu wanaandika kama burudani (hawa mara nyingi ni watu ambao hawana shida ndogo ndogo), kuna waandishi Wanaandika kama kazi, yaani ni sawa na wewe unavyo amka kwenda kwenye kampuni au ofisi unayo fanyia kazi. So kama unavyokuwa unafeel kuhusu kazi yako kuna waandishi nao wanafeel maandishi hivyo hivyo.

Ni vyema tupunguze kuwabeza sana waandishi kwa kuhisi ni wapoteza muda kuandika na kuanza kuwasapoti.

Uwe na siku njema.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
You said it all. Pamoja sana mkuu
 
Mmmh mkuu hii umetisha sana daah 🙏🙏🙏♥️♥️♥️
 
Ndo kwanza aaaa kimenuka🤣🤣🤣🤣
 
Mmmh hadi nmeogola 😌😌😌😌😌
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: +18

UTANGULIZI................

SURA YA 1.
MIMI NI NANI?


MZIZIMA,
Mvua zilizokuwa zimeambatana na upepo mkali zilikuwa zikiendelea kulisumbua jiji la bandari ya Salama, jiji la kale ambalo watu wa zamani walilijua kama mzizima. Mvua hizo ziliwafanya Tanesco wapate kisingizio kizuri kabisa cha kuweza kuukata umeme ambao ulikuwa unaimulika mitaa mbali mbali na kuonyesha umaridadi wake.

Kwenye chumba kimoja maeneo ya Kigogo Mwisho alionekana ndani mwanaume mmoja, kuonekana kwake kulidhihirisha wasiwasi na hofu ambayo ilikuwa imeugubika uso wake na simanzi ikauzidisha upole wa ile sura yake ambayo haikuwa ikionekana vyema huenda kwa sababu ya kukosekana kwa mwanga. Uso wake ulitoa taarifa ya kwamba maisha yake hayakuwa salama ndiyo maana alikuwa hana amani wala kuwa na utulivu wa kutosha, alikuwa ameketi kwenye mkeka ambao ulikuwa umetandikwa chini kwenye chumba kidogo cha hovyo ambacho kiligubikwa na joto kali kwa kukosa nyenzo mhimu za kupambana na joto. Sanjari na hilo udogo wa chumba nao ulichangia kwa kiasi kikubwa.
Mwanaume yule alijizoa kutoka kwenye ule mkeka na kusimama, alijisogeza kwenye dirisha dogo ambalo lilifunikwa kwa tambala kuu kuu lilolokuwa chafu, alifunua kidogo pazia hilo ili kujua kama nje kulikuwa na chochote lakini hakufanikiwa kuona jambo lolote lile zaidi ya radi ambazo zilikuwa inamulika kila wakati kwenye kiza totoro kilicho lifanya jiji hilo kuwa na utulivu ambao sio kawaida yake. Alirudi tena kwenye mkeka wake akiwa anatweta kwa jasho kutokana na joto kali huku akiwa anajifuta jasho hilo kwa kutumia shati lake ambalo lilikuwa mwilini.

Akiwa anaendelea kuhema kwa hesabu maalumu ambazo alizijua yeye na nafsi yake, alihisi kama kuna kitu kinamtekenya kwenye mfuko wake wa suruali, hapo ndipo akakumbuka kwamba kwenye mfuko huo alikuwa amehifadhi kisimu kidogo ambacho alikuwa amekifunga funga kutokana na uchakavu ambao kilikuwa nao. Aliipokea haraka simu hiyo ambayo namba yake haikuwa na jina na kuiweka kwenye sikio lake.
"Ondoka haraka kwenye hilo eneo, una dakika kumi na tano tu za kuyaokoa maisha yako, vinginevyo unakufa" sauti ya upande wa pili iliongea kwa msisitizo kisha simu ikakatwa. Alibaki kwenye mshangao mithili ya mtoto ambaye alikuwa ametelekezwa na mama yake mzazi huku akiamini kwamba alikuwa na usalama wa kutosha kwa sababu mama yake alikuwa karibu.

Alijizoa kivivu huku moyo wake ukiwa unamuenda mbio, alisogea kwenye ule mkeka na kuukunja upande wa juu ambapo eneo hilo kulikuwa na udongo ambao ulijazwa, aliufukua haraka haraka na kukitoa kimfuko cha plastiki. Alikifungua na ndani yake kulikuwa na pesa za kigeni maarufu kama dola huku pembeni yake kukiwa na bastola moja pamoja na kisu kimoja. Alizoa pesa haraka haraka na kuzitupia kwenye mfuko wake, bastola akaipachika kwenye kiuno chake huku kisu akikishika mkononi.
Alipafukia kama alivyokuwa amepakuta mwanzo na kuurudishia ule mkeka kwa mara nyingine tena kisha akanyanyuka na kuanza kutoka nje. Baada ya kufika mlangoni alikuwa amepoteza dakika tatu tayari, aliufungua mlango taratibu kisha akaangaza kila upande ili kuona kama angefanikiwa kuona kile ambacho alikuwa ameambiwa kinaenda kutokea lakini hali ilikuwa shwari kabisa hivyo akajitosa kwenye maji ya mvua na kuanza kutembea haraka haraka ili kuelekea kilipokuwepo kituo cha magari.
Alikunja kona ya kwanza akiwa anapishana na sauti ya kudondoka kwa maji, akakutana na uwazi ambao ulikuwa na mita kama kumi na tano, sehemu ambayo ilimshtua kidogo kwa sababu moyo wake ulimuenda mbio isivyokuwa kawaida. Alitembea haraka haraka ili aweze kulivuka eneo hilo salama huku kwenye mkono wake kisu akiwa amekishikilia vyema, ila hakupiga hatua hata kumi akahisi kabisa kulikuwa na harufu ya mtu ndani ya eneo hilo hali ambayo ilimfanya kupunguza mwendo na kumfanya aanze kutembea taratibu.

Aligeuka kuangalia nyuma yake, hakuona kitu zaidi ya anga ambalo lilikuwa linamcheka hivyo akahitaji kuendelea na safari yake tena lakini nafsi iligoma kabisa, moyo wake ulikuwa mzito na hakuwa mtu wa kuupuuzia huo mlango wake wa sita ambao ulikuwa wa hisia. Alishuka chini kama anajilaza kifudi fudi lakini hakufika chini kwa sababu ule mkono wenye kisu ndio ambao ulitangulizwa kisu ndicho kikafika chini na hata baada ya kufika pale chini kwa mkono wake hakuzubaa, alijigeuza kwa sarakasi kwa kuuviringisha mwili wake hali ambayo ilimfanya atue pembeni.

Mahesabu yake yalikuwa sahihi kwa sababu wakati anashuka pale chini, juu yake kilipitishwa kisu kutoka kwenye mikono ambayo ilionekana kuwa na nguvu kubwa na lengo la mtu huyo halikuonekana kuwa kumzimisha tu bali alikuwa anahitaji kuondoka na nafsi yake moja kwa moja. Hata baada ya kutua pale chini hakuzubaa kwa sababu alijua huenda akampa adui nafasi nzuri ya kuweza kufanikisha jambo lake kitu ambacho hakutaka kiweze kutokea kwake yeye ndiyo maana alijiviringisha kwa sarakasi na kutua pembeni. Kujiviringisha kwake kulimfanya kulikwepa buti zito la ngozi ambalo lilikuwa limeshushwa na mwanaume ambaye alionyesha kuwa na uhasama naye mkubwa mithili ya mtu ambaye alimuibia mkewe, buti hilo kama lingefanikiwa kutua kwenye mgongo wake basi asingefanikiwa kutembea tena kwenye maisha yake yote.

Kiza kinene kilimfanya mwanaume huyo ashindwe kumtambua mwanaume ambaye alikuwa amekuja mbele yake ila mwanga wa radi ulimumulika mtu huyo ambaye bila shaka alikuwa ni mweusi usoni akiwa kwenye ghadhabu isiyo pimika. Aliukunjua mkono wake ambao ulikuwa na kisu kwa sababu alijua kwamba anatakiwa kufa wakati huo asipo yatetea maisha yake, hakupata muda wa kutosha wa kupiga tathmini juu ya uwezekano kama alikuwa anamfahamu mwanaume huyo kwa sababu alikuwa anamjia kwa kasi pale alipokuwepo huku mabuti yake yakiwa yanapiga piga kwa nguvu kwenye maji ambayo yalikuwa yametuama chini.
Miguu yenye nguvu miwili ilikuwa inakuja kwenye uso wake, kama bahati tu, tope lililokuwa chini lilimsaidia kuteleza kidogo na kurudi nyuma hali ambayo iliifanya miguu hiyo kumkosa na badala yake akarushiwa maji machafu usoni ambayo yalimuingia kwenye macho. Mtetemo wa ardhi aliusikia vyema baada ya ile miguu ambayo ilimkosa kutua chini na kukita kwa nguvu. Aliyafumbua macho yake haraka ili kujilinda, alichelewa kwenye mahesabu, ngumi ilizama kifuani na kumfanya ahisi kama kuna mtu alimpasua na shoka.

Ndiyo kwanza kabisa tunaufungua utangulizi wa simulizi hii mpya ya NAFSI ZILIZO TELEKEZWA. Hii ni simulizi bora zaidi kati ya simulizi zangu tisa za kijasusi ambazo nimeziandika.
Ndani yake utakutana na stori kali zilizo simama, utakutana na watu kutoka mataifa makubwa na mashirika makubwa ja kijasusi duniani hususani IRINA ESPANOVICH, mwanamama kutoka ndani ya KGB ambayo alikuja akaiweka Tanzania kwa mkono wake baada ya kutoroka nchini mwake akiwa anatafutwa kwa nguvu na Moja ya mashirika makubwa duniani, shirika la kijasusi la Uruai KGB kwa kuwasaliti wenzake na kufanya Umoja wa nchi za kisovieti kudondoka mwaka 1991.

Kutoroka kwake ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya hatari ndani ya TANZANIA ambayo ilifahamika kama LUNATIC SOCIETY. IRINA alifanikiwa vipi kuwakimbia watu wa kutisha hao wa KGB kwa kuwasaliti mbele ya CIA halafu akafanikiwa kufika Tanzania?
Hiyo jamii ambayo aliianzisha ilikuwa inajishughulisha na nini hasa na mwisho wake ulikuwaje?
IRINA ni nani hasa na alifanya usaliti wa namna gani mpaka KGB wamsakame kila kona ya ulimwengu huku yeye akipotelea Tanzania?

Hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA Zina maana ipi na ni NAFSI za nani na nani?

Maswali ni mengi lakini ungana NAMI wakati huu uweze kusoma simulizi yangu bora kuliko zote ambazo nimeziandika. Ipo tayari kuanzia muda huu.

Bei yake ni shilingi 6000 tu za kitanzania unajipatia nakala yako kwa mfumo wa softcopy (pdf) kwa kulipia kwa namba hizi hapa.

0621567672 (HALOPESA)..... WHATSAPP

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

0689440143 (AIRTEL MONEY)

Zote jina ni FEBIANI BABUYA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…