MSIMAMIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Mkoa wa Iringa, Bi. Nuru Sovella, amesema kuwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeweka mazingira rafiki na wezeshi kwa watu wenye ulemavu ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo mkuu, Bi. Sovella ameeleza kuwa watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona, wasiokuwa na mikono, watu wafupi wa kimo, pamoja na makundi mengine yatapewa kipaumbele maalum siku hiyo, na hawatalazimika kupanga foleni vituoni.
Aidha, aliwahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo muhimu wa kumchagua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.
Kwa upande mwingine, Bi. Ndovela alitoa ufafanuzi kwa wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura akifafanua iwapo mtu alijiandikisha katika Daftari la judumu la wapiga Kura lakini amepoteza kitambulisho chake, bado anaweza kupiga kura kwa kufika katika kituo alichojiandikishia akiwa na kitambulisho cha taifa (NIDA), pasipoti au leseni ya udereva yenye jina linalolingana na taarifa zake kwenye daftari.
Wanajaribu kulipa attention hili igizo lililopuuzwa vibaya sana na watu ,kwa kutoa matamko utadhani ni vitu vipya kumbe vilishakuwa vinafanyika awali yote hayo ni kujaribu kuhadaa watu kuwa kuna uchaguzi wakati kimsingi ni uchafuzi.