Incomplete Hesbl

Rayzuh

Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
13
Reaction score
4
Nmekuwa very disappointed baada ya process nzima ya uombaji mkopo wa elimu ya juu kuwa incomplete na imeandkwa kureapply mpaka november 1 2019 hadi november 11 2019 ambapo muda wa masomo kuanza n tayari.
 
Wasomi wa siku hizi mnakera sana, kichwa cha mada kimeandikwa kea kingereza yaliyoandikwa ndani kingereza na kiswahili duh.

Hesbl ni nini ?
Nmekuwa very disappointed baada ya process nzima ya uombaji mkopo wa elimu ya juu kuwa incomplete na imeandkwa kureapply mpaka november 1 2019 hadi november 11 2019 ambapo muda wa masomo kuanza n tayari.
 
Nmekuwa very disappointed baada ya process nzima ya uombaji mkopo wa elimu ya juu kuwa incomplete na imeandkwa kureapply mpaka november 1 2019 hadi november 11 2019 ambapo muda wa masomo kuanza n tayari.
 
Mkuu embu weka wazi ,umeona kwenye account yako ya mkopo au umeona wapi ?
 
mkuu mbona unawatisha waombaji. hii taarifa umeitoa wapi? mbona unazua taharuki wakati tangazo la bodi leo limeweka utaratibu wazi kuwa mpk tarehe 30 jumapili ndipo watamaliza kupitia fomu zenu za maombi then kwa watakaokuwa na mapungufu katika fomu zao wata re-apply kuanzia jumatatu
 
Ok...kwahyo mpaka itakapofikia jpili kunaweza kukawa na updates kuhusu mikopo sio!?
 
kipindi hiki ni noma sana , unajikuta umefaulu lakini utalia majonzi mengi utaona serikali imekutenga , utasahau shangwe zote ulikuwa nazo pale majibu yalipotoka kuwa umefaulu uyajuta sana lakini kumbuka wote tumepitia hapa hivyo wewe hautakua wa kwanza.
 
TAARIFA MUHIMU KWA WAOMBAJI MIKOPO KWA 2019/2020

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwajulisha waombaji wote wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa kwa sasa HESLB inaendelea na kazi ya uhakiki (verification of online-submitted applications) wa maombi yaliyowasilishwa ambayo itakamilika Jumapili, Septemba 29, 2019.

Baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki, HESLB itatoa fursa ya siku nne, kuanzia Jumatatu, Septemba 30 hadi Alhamisi, Oktoba 3, 2019 kwa waombaji mikopo ambao maombi yao yatakuwa yamebainika kuwa na upungufu kufanya marekebisho.

Taarifa hii inatolewa kufuatia HESLB kupokea maoni na maswali kupitia barua pepe na simu kuhusu hatua iliyofikiwa katika uhakiki na uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu yaliyowasilishwa HESLB.

Waombaji mikopo wote wanashauriwa kutembelea tovuti yetu (www.heslb.go.tz) au kuingia katika akaunti zao waliozoombea mkopo kupitia mfumo wa uombaji mkopo (www.olas.heslb.go.tz) kuanzia Septemba 30, 2019 ili kupata mwongozo wa kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao. Baada ya kuingia, watapata ujumbe iwapo maombi yao yamekamilika au yanahitaji marekebisho.

HESLB imejipanga kuhakikisha kazi yote ya uhakiki na uchambuzi wa maombi yote ya mikopo inakamilika ifikapo Oktoba 6, 2019 ili wanafunzi wahitaji wapangiwe mikopo, wapate taarifa na fedha za mikopo zitumwe vyuoni kabla ya vyuo kufunguliwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.hesl.go.tz).

Mwisho.



Imetolewa na:

Abdul-Razaq Badru,

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Source; https://www.heslb.go.tz/Post/view_post?post=11
 
Hiyo
 
Manzi wangu kanisumbua sana na hii taarifa, namwambia bado yeye anadai wenzake washaona taarifa zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…