*INAUMA SANA*
Kijana mmoja alifanya maamuzi ya kumpeleka baba yake ambaye, alikuwa amezeeka sana, kwenye makazi maalumu ya kulelea wazee ya Kanisa Katoliki.
Kijana alifanya hivyo, baada ya kushauriwa na mkewe, aliyekuwa akiona kero kumlea baba mkwe wake nyumbani kwao.
Ofisa katika sehemu ya mapokezi, alimuomba mzee huyo achague chumba kama anataka chenye TV na Kiyoyozi, au la; mzee akasema hahitaji chumba chochote Chenye TV wala Kiyoyozi.
Mwanaye alipokwenda kwenye Gari kuchukua begi la baba yake; mkewe aliyekuwa muda wote kwenye gari, akasisitiza kuwa kijana amwambie huyo mzee wake asiwe anarudi nyumbani kabisa, hata siku za Sikukuu, kwa sababu yeye hataki usumbufu wowote wa kumhudumia.
Kijana huyo ambaye ni mtoto wa pekee kwa mzee yule, alishangaa alivyorudi na mizigo ya baba yake, na kumkuta mzee wake akizungumza kwa furaha na bashasha na Padre, tena wakionekana kufahamiana sana. Walionekana wakiongea kwa kukumbushana mambo ya zamani ambapo, mzee alionekana mchangamfu isivyo kawaida.
Mtoto akamuuliza Padre, "Unafahamiana na baba yangu?"
Padre akajibu, "Ndiyo, namfahamu sana mzee huyu. Ni mtu mwema sana; alikuja hapa miaka 30 iliyopita, tukampatia mtoto yatima wa kiume akamlee, maana Mtoto huyo alitelekezwa. Na kwakuwa yeye na mkewe hawakuwa wamebahatika kupata mtoto, wakamchukua."
Mabegi aliyokuwa kayashika mkononi kijana yule yalimdondoka bila kujijua. Alibaki ameduwaa huku machozi yakimtoka. Kumbe baba aliyemlea kwa wema na upendo hadi naye akafanikiwa maishani, hakuwa baba mzazi, alikuwa ni mlezi tu aliyemsitiri. Lakini yeye ameamua kumuondoa nyumbani kwake kwa sababu ya ushauri wa mke.
*USIKURUPUKE USIMFANYIE MTU KITU USICHOPENDA KUFANYIWA...*
Umejifunza nini mdau??
Matukio ya ajabu Duniani..