Inasikitisha! Ubadhirifu mkubwa TANAPA

Status
Not open for further replies.

mwakibolo

Senior Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
163
Reaction score
47
Rais wangu Magufuli hebu mulika TANAPA kwa jicho la pili. Hili suala eti Tembo anafungwa kifaa kitakachokuwa kinawa monitor ili wasiibiwe linashangaza! Kifaa chenyewe ni mil 30 kwa Tembo 1.

Hivi Allan Kijazi umekosa ubunifu mwingine na katibu mkuu wako? Kwa uelewa wangu mdogo hamuwezi kuwafunga Tembo wote hicho kifaa, na bei yake sio hiyo pia. Hata kama ni hiyo kuna uchakachuaji mtafanya mpige cha juu.

Kwani nini kazi ya askari wanyama pori? Basi wasiwepo ili mfunge kila mnyama hicho kifaa.

==============
 
Kama Ngorongoro Conservation Area Authority(NCAA) wanahoteli za kitalii kule ila vikao vingi wanafanyia Arusha hapo achana viongozi karibia wote kwenda Arusha kuanzia ijumaa hadi J3 asbh kula weekend na mashangingi ya mamlaka
 
Tooobaaa huu sasa uwendawazimu mil 30:what::banghead:
 
Kama Ngorongoro Conservation Area Authority(NCAA) wanahoteli za kitalii kule ila vikao vingi wanafanyia Arusha hapo achana viongozi karibia wote kwenda Arusha kuanzia ijumaa hadi J3 asbh kula weekend na mashangingi ya mamlaka
Ikibidi Mheshimiwa Rais upitie upya ajira zinazotolewa hapo NCAA! nyingi za ajira hizo ni hongo haswa za ngono, vimada ni wengi wameajiriwa na baadae kusomeshwa na fedha za shirika (fedha za umma) na hata hivyo haitoshi utaalamu wa kiuhifadhi hawana ni wamejazana ndugu, mjomba, shangazi yaani mpaka inachekesha! wakati kuna vijana wanaelimu ya kutosha kuhusu uhifadhi lakini hawapewi ajira kabisa hiushia kwenye interviews tu na mwishowe ni hao vimada ghafla wako nadani ya kombati! Mheshimiwa Rais tafadhali vamia na hilo shirika ujionee uozo na madudu!
 
Mleta mada, sema wewe bei ya hivyo vifaa ni sh ngapi? Halafu acha kuongopa. Vifaa hivyo havikununuliwa na tanapa, isipokuwa taasisi ya kuhifadhi tembo inayoongozwa na dk. Kikoti. Majungu yako kwa TANAPA hayana ukweli wowote. Tafuta jingine. Hili umechemka mbaya.
 
magufuli anaonyesha kuwa nchii hii sio maskini, ila wananchi ndio maskini utajiri ni wa serikali ya ccm na watumishi wake.

Kitu kikiwa ni cha kiserikali tu bei ni mara kumi ya mtaani.

"maskini wanateseka wanakatwa kodi, hazina inajaa matumizi ndio hayo, ila jamaa wanajiita serikali wakija utasikia bungeni wanapitisha chai ya office mill 20, utadhani kitumbua cha serikalini ni Sh laki moja"
 
Mod ondoeni uzi huu wa uongo. Hakuna kifaa kilichonunuliwa na Tanapa. Huu ni msaada tu wa taasisi iliyo kwenye mapambano ya kuwalinda tembo. Uzi wa aina hii uliojaa uongo unashusha hadi ya JF.
 
Kwa hili hata mimi mwana ukawa nakupinga. Vile vifaa vinafungwa kwa tembo mmoja katika kila familia ya tembo, usidhani tembo wanaishi kama nyumbu! Pale utakuta kuna hadi binamu na wakwe.
 
Huu ni uongo wa waz.kabisa.mtoa mada una kisasi na mr Kijaz.mim siipend ccm lakin kwa ili hapana ivyo vifaa ni msada vilitolewa.
 
Unaulizwa kifaa bei gani hujibu, unaambiwa vifaa vimetolewa msaada labda utaomba thread ifutwe sasa.
 
There is no free lunch... ..misaada yote tunairudisha. Kama tanapa na ncaa wanapiga pesa usishangae, CAG inabidi awakague
 
TANAPA na NCAA kumeoza hasa NCAA.. Haya mashirika yanapaswa kusafishwa kwa kuanza na bodi zake.
 
Huu ni uongo wa waz.kabisa.mtoa mada una kisasi na mr Kijaz.mim siipend ccm lakin kwa ili hapana ivyo vifaa ni msada vilitolewa.

Usipotoshe...hivyo vifaa TANAPA wenyewe ndo walisema vimenunuliwa kwa bei tajwa....na wakasema zoezi litaendelea kulingana na upatikanaji wa "njuruku"
 
hahahaha kwel kila mbuzi anakula kwa uref wa kamba yake.....


askari pori watalewa tu
 
tanapa nako kuna mianya ya kupiga deal, kweli bongo balaa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…