Nakusoma bila miwani!!Gosh ni kweli usemayo Sio njema kabisa Nguli haileti picha nzuri katika mahusiano ..Ila siku akija Denzel Washington nitaomba muzee anipe chance nikamkumbatie kidogo tu .....sijui mapromota watamleta lini ?
Pole Nguli kama yamekukuta..
Exactly, I concur with you....huo ni uzalilishaji wa kijinsia. Hivi unajua wanawake wanapenda kusifiwa wao tu, jaribu kuangalia movie naye, then umuone demu bombo sana, na useme duh..huyu demu mkali ile mbaya utaona moto wake, au umsifie msichana anayemjua utakoma kuringa!....ahhh, huo ni unyanyasaji wa kiakili bana, haivumiliki! ...ni sawa na mkeo kutwa kucha anasifia kupita kupitiliza wanaume wa kwenye tamthilia za televisheni kina "Juan Miguel" au "Brad Pitt", as if wewe ni pakashume tu hapa duniani!
Umejitihadi ukamtimizia haja yake ya kumpeleka out kwenye concert ya maisha yake kumwona mwanamuziki aliyetamani maisha yake yote kumwona/kuwaona. Mara anatambulishwa mwanamuziki jukwaani zinapigwa fataki pale za kuonyesha star anaingia mara anaanza kulia akimwona tu anazimia mfano mzuri cheki clips za Michael Jackson. Akizinduka anang'angani kwenda mbele kucheza naye anazuiwa na walinzi anaforce kwa kujigaragaza chini mpaka star/mwanamuziki anasema mwacheni aje akifika pale jukwaani anamkumbatia na kuanza kulia. hivi uta react vipi katika hali kama hii. Akirudi toka jukwaani utaendelea kutabasamu na kucheza naye tuu??? Ni swali tu tu shee mawazo labda mimi nakuwa mshamba hapa.