IFUNDA TECHNICAL ALUMNI Special Thread.

NDESSA

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
1,946
Reaction score
1,800
Ndugu wahitimu wa Ifunda kwa miaka yote tangu shule ilipoanzishwa napenda kuwajulisha kuwa tunao Umoja wa wahitimu wa Ifunda unaotambulika kama Ifunda Technical Alumni Association(ITAA) na tulipata usajili kutoka mamlaka ya usajili wa vyama Wizara ya mambo ya ndani mwaka jana,Tumekuwa na utaratibu wa kukutana wanachama kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuendeleza shule ya Ifunda lakini pia kuweza kuwaleta watu pamoja na kufahamiana ili kupanua mtandao wa wanaifunda popote walipo,kuna mipango mingi ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji hususani mradi wa kuwapatia Ifunda kisima cha maji safi tayari kuna michango ya wanachama na wadau wengine wanaendelea kuchangia mpango huu uliozinduliwa mapema mwaka jana mwishoni DSM na msukumo mkubwa wa kufanya mradi huu ni kutokana na kilio cha wanaifunda cha kuwa na chanzo cha maji kisicho cha uhakika yani Lyandembela,Kutokana na ratiba ya vikao vya umoja kwa mujibu wa katiba yetu tuliazimia kukutana jumapili ya tar 01 sept 2013 na Uongozi umependekeza kikao hiki kiwe tofauti kidogo yani iwe Get together part ambapo tumepanga kufanyia pale Msasani Beach Resort ya JKT kuanzia saa 6 mchana kutokana na utofauti wa mahali husika kila mmoja atatakiwa kulipa kiingilio kiasi ya sh Elfu tano tu (5,000) pia utapata na kinywaji,WOTE MNAKARIBISHWA SANA, Nimetoa maelezo japo kwa ufupi kwa sababu kuna ambao hii ni habari mpya kwao tumekuwa tukitumia vyombo vya habari kutangaza shughuli zetu hususani TBC1,Couds,Capital,Blogs mbalimbali na fb, wakati mwingine nitaandaa maelezo marefu sana kwa sababu ni vigumu kwa jiografia yetu wote kuweza kukutana pamoja ikizingatiwa kuwa tumekuwa tukikutana sana DSM,
mnaweza pia kutembelea page yetu ya facebook IFUNDA TECH, ALUMNI ASSOCIATION(ITAA)
Imetolewa na DAMACENT MICHAEL (KATIBU MKUU MSAIDIZI ITAA)
BOX 35935
DSM
Mob; 0752 513 154
 
Vijana wa IFUTESCO AKA WANYAMA WAZEE WA ULANZI: Ifunda pamechangamka now days pamekuwa nji kabisa baada ya ujenzi mpya wa barabara na utanuzi wa parking,lory za mizigo zinazokwenda nje zimepachangamsha sana baada ya kifanya ni kituo cha kupumzika,guest za kumwaga kwa ajili ya akina niangusage sambi sako mwenyewe
 

Mkuu ni kweli pamebadilika tofauti na zamani,kuna vitu vingi vya kukumbuka Ifunda the Glorious! Karibu sn
 
I wish ningekuwepo na nilitamani sana kuudhuria sema nimesafiri kikazi! I wish all the best kwa watakaopata nafasi ya kuudhuria
 
Yale maji ya DANIDA kutoka chanzo cha maeneo ya ndanindani Kibaoni yamekauka? Nakumbuka mwaka 1989 mwalimu mmoja aliyeitwa Nyirenda alisimamia ule mradi na tatizo la maji lilipungua kiasi kikubwa, maji yalikuwa yanaingia tangi la Kibaoni kwa GRAVITY.
 
I wish ningekuwepo na nilitamani sana kuudhuria sema nimesafiri kikazi! I wish all the best kwa watakaopata nafasi ya kuudhuria

Mkuu karbu wakati mwingine ukipata nafasi kwa sababu hiki kitu ni endelevu,Asante.
 
Yale maji ya DANIDA kutoka chanzo cha maeneo ya ndanindani Kibaoni yamekauka. Nakumbuka mwaka 1989 mwalimu mmoja aliyeitwa Nyirenda alisimamia ule mradi na tatizo la maji lilipungua kiasi kikubwa, maji yalikuwa yanaingia tangi la Kibaoni kwa GRAVITY.

Mkuu bila shaka unaongelea Kivalali yale yapo lakini kwa uchache hayatoshelezi,Lyandembela ndio tegemeo lakini napo ile ni surface water sio reliable pia hakuna miundombinu wezeshi kama mifereji ya kupeleka maji kwenye pump hvyo shule kwa kushirikiana na Manispaa ya Iringa walifanya survey pale wakaandaa BOQ ya 16 Mil. Kama fedha ya kutengeneza pale,mwaka jana tulituma timu ya watu 6 kutembelea shule kujionea hali ilivyo mrejesho wa safari ilikuwa kwamba kilio chao ni Maji,Tulipofanya kikao cha members waliohudhuria Octoba 28 mwaka jana White Mark Hotel wataalam wa Geology walishauri kuwa maji ya uhakika ni ya visima virefu hvyo tukakubaliana kutafuta pesa ya kuchimba kisima pale,Karibu.
 

sawa tupo pamaoja mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…