Nicodemas Tambo Mwikozi
JF-Expert Member
- Aug 13, 2016
- 663
- 1,047
Ni wakati ambao Alarm iliotumika kuniamsha ilikua jogoo linapowika, saa yangu ya mkononi ilikua kivuli changu, kadri kinavyokua kirefu au kifupi na kuhama upande niliweza kubaini sasa ni saa ngapi
Jua lilipozama liliashiria ukomo wa siku na kwa mjibu wa sheria za nyumbani nililazimika muda huo kuwepo nyumbani kuhakikisha kama kuku wote wamerudi na kufunga banda lao Baada ya kufunga ilikua ni marufuku kutoka tena nyumbani baada ya jua kuzama na kiza kutanda. Kuzurula usiku ilikua ni alama ya watoto wasio na maadili.
Msimu wa kupapalilia mashamba au kuvuna mazao ni wakati niliouchukia kuliko nyakati zote kwani baada ya jogoo kuwika tuu ilikua ni kiashiria safari ya kwenda shamba imewadia
ulikua ni wakati wa kuachana na usingizi na kuanza safari ya takribani kilometa 5 kwa mguu kutoka kijijini kueleke mashambani huku jembe begani na dumu la maji. Safari ya kurudi tena kijijini ilikua ni saa 12 jioni baada ya kazi nzito.
Bado nakumbuka vema tuhuma zangu kutoka kwa mama Nico wewe ni mvivu saana ukazane kusoma hapo ni baada ya watu wote kumaliza vipande vyao walivyogawiwa kupalilia au kuvuna na kulazimika kuja kumalizia eneo langu ambalo bado sijamaliza ili safari ya kurudi nyumbani ianze.
Haya yote hayajafanya niandike kilichonitesa ni wakati wa kurudi nyumbani jioni, njaa ilikua kali na uchovu Mwingi magari yalitupita na mama aliposimamisha kuomba lift tulinyimwa mara nyingi zaidi, kuliko zile tulizopewa.
Jambo lililoniumiza zaidi ni gari ambayo alikuwemo dreva tuu lakini hakusimama kutupa lift na nafasi ilikuwepo katika gari. Tuliendelea kutembea umbali mrefu mpaka kufika kijijini kwetu, na mkifika watoto wa kike na mama walipitiliza kupika pamoja na uchovu mwanamke ana nguvu sana.
Kutokana na kunyimwa lift wakati nimechoka nikitokea shamba niliapa kuweka nadhiri Kua nikiwa mkubwa nikinunua gari stamnyima mtu yoyote lift azimio hili nililiweka kichwani mwaka 1998 nikiwa darasa la tano.
Miaka 15 badaye mwaka 2014 nilitimiza ndoto yangu ya kununua gari. kwanza kabla ya kununua gari niliwaza nikinunua Vits au Ist stawapa watu wengi lift nikaamua kununua gari aina Noah ambayo nikiwa peke yangu nitawapa lift hata watu 11 moyo wangu ufrahi.
Nikanunua gari azimio langu la kwanza ikiwa mchana nitampa lift mtu yoyote yule ila kamwe stamuacha Mama yoyote mwenye mtoto barabarani kama ni usiku stawapa lift wanaume labda watoto kutokana na sababu za usalama.
Ndoto yangu ikatimia nikafrahi likizo nilipooenda kijijini Mpui jioni nikawa natoka na kuelekea upande wa mashambani Lengo kuwapa lift akina mama na watoto wanaotoka shambani
Moyo wangu ukafrahi nakajihisi nalipa deni kubwa kila akina mama waliposhuka na kunishukuru nilikumbuka mama angu alivyofanya pia enzi nakua. Kila nilipoona watoto wakikimbilia kupanda nilikumbuka wakati wangu niliyoona ahuheni kwa kupata lift nilifrahi nikatabasamu Nikajihisi natua mzigo mzito moyoni baada ya miaka Mingi
Kwa marafiki zangu wenye magari tuwasaidie mama zetu tunaowakuta barabarani wanapitia mengi, magumu wengine wanawahi wagonjwa, misiba, biashara, na mambo mengi wao ndio waliishikilia jamii zetu
Haikugharimu sana kupoteza dakika moja kumpa lift Mtu pia ni baraka ndogondogo unapomrahisishia mwenzio safari ni tendo la upendo na la baraka
Leo nimekumbuka tuu miaka kadhaa nyuma lift ilipokua Ni farija katika Moyo wangu basi faraja hiyo nami nagawa tugawane faraja na wezentu kwa kidogo tunachopata.
"My dear I need private with you, but u take a lot of people tunaposafiri why lakini? Do you know them? " sauti hii ilipopenya kwenye masikio yangu ulikua mwiba Mkali.
Kauli hii stafafanua kwa leo
Wasalaamu.