Nadhani Crashwise , Masuke , Saint Ivuga na watani wengine wanaweza wakatueleza nini kimeisibu Simba TV
Mimi kwangu Tanesco wamekata umeme siku mingi, hivi bado haijaanza?
mimi nafikiri hawana hela za kulipia kodi ya bandari au labda bado inatengenezwa au imeshauzwa na wajanja au wasahau walipoiweka au aise nimeishiwa na sababu hebu wacha tuwasikilize jamaa.:nerd:
Vipi bado hujashuka kwenye ndege? Hata kama bado hujashuka mbona hutupi habari za Okwi kama amekuja au la?Kesho ni tarehe 9,binafsi nitasafiri na Precision kutoka Mwanza to Dar,na Flight nitakayopanda nimesikia itaanzia Entebbe kama Kamwaga atakuwa ameongea neno la kwanza la ukweli naweza kuwa na Okwi kwenye board kesho,let me wait and see.
Mana'ke I real miss him,toka imeanza kusemwa atakuja-atakuja,simuoni aisee!
ni tv iliyokuwa ndani ya tv ya clouds,ilizinduliwa kwa mbwembwe nyingi,Mawaziri na watu wenye heshima zao walishiriki kuizindua ,tena kwa vinywaji na pilau ya kutosha,wakadai wao ndo wa kwanza kumiliki tv hapa bongo,wakadai wamebakiza kuzindua redio tu.Lakini tv hiyo imepotea ghafla kama popobawa.wahusika hebu tusaidieni majibu,kina shafii,rage,kamwagamwaga mpo!?:A S-confused1::A S-confused1: