Hypertension

Juandeglo

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2014
Posts
1,041
Reaction score
2,815
Habarini wanajamvi.

Moja kwa moja kwenye mada. Je ugonjwa wa pressure kupanda unaweza sababisha kuchanganyikiwa? Mgonjwa ameugua miaka minne sasa. Amekua akitumia dawa za hospitali kwa miaka yote hiyo tajwa.

Sasa hivi karibuni hali imebadilika akawa wa kulala tu hawezi fanya chochote. Chakula mpaka abembelezwe. Yeye yuko kijijini Same huko hospitali zinaoperate on weekdays sio weekends. Anaongea maneno yasiyoeleweka kama yuko confused. Je ni pressure tu au yumkini kuna tatizo lingine?

Please msaada ndugu zangu
 
Ni sahihi,hypertension(presha ya juu) ina uwezo wa kumfanya mtu achanganyikiwe na kuwa kichaa kabisa pamoja na kupata stroke.

Hata Baba yangu alichanganyikiwa na kuwa kichaa kabisa na pale KCMC madaktari wakasema imesababishwa na hypertension.Matibabu yake ni hadi kwenye hospitali za vichaa kama vile Mawenzi.

Baba yangu alitibiwa Mawenzi na akapona hilo tatizo la akili kabisa ila ni lazima vyote vitibiwe,yaani hiyo presha pamoja na hilo tatizo la akili.
 
Poleni sana mleta mada, ngoja waje kukupa muongozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…