KWA NINI UTUMIE HYDROPONIC FODDER KATIKA UFUGAJI WENYE TIJA
1. Ni rahisi kuotesha
2. Zinaota kwa muda mfupi
3. Zitakupunguzia gharama za chakula cha kuku
4. Zina wingi wa protein na vitamin, hivyo huongeza utagaji wa kuku na kinga za magonjwa
5. Zinapunguza uwezekano wa magonjwa yatokanayo na vumbi
OKOA 50% YA GHARAMA ZA MALISHO KWA KUTUMIA HYDROPONIC FODDER
Imethibitika kwamba unaweza kupunguza gharama za malisho ya mifugo( kuku, sungura, ngombe, mbuzi, kondoo), kwa kutumia hii sayansi
Hydroponic Fodder ni mmea wenye wingi wa virutubisho unaozalishwa kwa siku 5-7, kwenye trey maalumu,
Sayansi hii ni rahisi sana, inatumia eneo dogo na malighafi nafuu
Kilo moja ya nafaka( ngano, mtama, mahindi, uwele ) inakupa kilo kilo 8 hadi 10 za chakula chenye virutubisho lukuki.
Elimu ya uoteshwaji wa hydroponic fodder imetolewa kwenye kitabu cha MAPINDUZI YA UCHUMI NA UFUGAJI KUKU. ambacho ni kitabu cha bure, kilichoandikwa na Comrade Ally Maftah.